GET /api/v0.1/hansard/entries/1370733/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1370733,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370733/?format=api",
"text_counter": 304,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Tulienda pia mpaka Kaunti ya Uasin Gishu tukiendelea na majukumu ambayo tuliyopewa kufanya. Kwa sababu Maseneta wamekua na majukumu mengi, ni vizuri warudi sehemu zao wanazowakilisha ili kupumzika halafu warejelee maswala yao mwaka ujao kwa kasi. Ikumbukwe wazi kwamba mwaka huu, nchi hii ilipata kiangazi na pia kulikua na maandamano. Huu mwaka tena ndio tumepata mafuriko. Yote tisa, kumi ni kwamba, ni vizuri angalau Seneti hii ichukue likizo ili waangalie haya mambo yote kwa undani, ili mwaka ujao tuweze kuangazia sheria ambazo zimeletwa Bunge hili na pia kushukuru Maseneta ambao walichangia hizi sheria. Bi. Spika wa Muda, kwa sababu kuna ndugu zangu wanaotaka kuchangia na kuongea mengi, sitaongea zaidi ya hapo, lakini ninawatakia Wakenya Krisimasi yenye mafanikio na mwaka mpya ambao watapata mambo mengi yatakayopeleka nchi yetu mbele kabisa."
}