GET /api/v0.1/hansard/entries/1370755/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1370755,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370755/?format=api",
    "text_counter": 326,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bi. Spika wa Muda. Naunga mkono kuhairisha kikao ili tuende kwa msimu Krismasi. Tangu nijiunge na Seneti, najivunia kukamilisha mwaka mmoja. Nilikutana na marafiki, Maseneta 67, Spika na wafanyakazi wanaotusaidia katika Seneti kama vile clerks na secretaries . Pia nimejifunza mengi kutoka kwa Senate Majority Leader, Seneta wa Kericho County, Sen. Cheruiyot, Sen. Sigei, Sen. Okiya Omtatah, Sen. (Dr.) Khalwale na Sen. Oketch Gicheru kutoka Migori County. Kwa hiyo, nashukuru. Nawaambia watu wa Kenya kuwa tukiwa hapa tuko na Azimio na Kenya Kwanza. Lakini, tukitoka nje tunakunywa chai pamoja. Nilifikiria kuwa tutakuwa na vita lakini hakuna vita. Embu County tuko na four sub-counties ; Mbeere North, Mbeere South, Manyatta na Runyenjes. Nawapenda sana watu wa Embu kwa sababu mlinipatia kura kati ya watu 12 ambao walikuwa na mali. Ijapokuwa sikuwa na chochote, mlinipa kura zenu. Kwa hiyo, kwa kipindi kilichobakia, nawaambia watu wa Embu kuwa tuko pamoja. Makanisa yote yaendelee kuniombea ili niwe na nguvu yakuendelea kuwatetea katika Seneti. Pia, nashukuru chama cha Democratic Party ambacho kiko kwa muungano wa Kenya Kwanza. Tunaunga mkono Rais na Makamu wa Raisi ili tuwe pamoja. Mwisho, nawatakia Krismasi njema, mwaka Mpya wenye mafanikio pamoja na siku ya Jamhuri njema. Pia, kwa wale walioenda Rwanda, nawahimiza tuwe kitu kimoja ili tuwe mashujaa wenye nguvu. Asante Bi. Spika wa Muda. Naunga mkono."
}