GET /api/v0.1/hansard/entries/1370769/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1370769,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370769/?format=api",
"text_counter": 340,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Githuku",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13595,
"legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
"slug": "kamau-joseph-githuku"
},
"content": "Hoja hii ambayo imeletwa na Kiongozi na Kinara wa Wengi kati Bunge hili la Seneti. Mimi ni kati ya Maseneta ambao wamepiga kipindi kwanza katika Seneti hii. Ninashukru kwa sababu nimesoma mengi kupitia kwa uongozi ambao umekuwa katika Seneti hii. Hata hivyo, mimi ni kati ya Maseneta ambao wamemaliza kipindi hiki wakiwa na majonzi na masikitiko makubwa kufuatia shida na matataizo ambayo yamekuwa yakikumba watu wangu. Tunapoongea watu wangu katika Kaunti ya Lamu wana kilio kikubwa kwa sababu ya mauaji ya kiholela ambayo yamekuwa yakiendelea katika Kaunti ya Lamu. Serikali sasa inafaa kutilia mkazo ili kuona ya kwamba hakuna mauaji tena katika Kaunti ya Lamu. Bi. Spika wa Muda, tunaelekea msimu wa Krismasi ambao ni wa watu kusherehekea. Sitaki kusema ya kwamba Lamu kuna furaha. Ni kwa sababu sasa hivi, kuna shida na matatizo kufuatia mauaji yaliyofanyika huko. Mafuriko pia yameathiri watu wangu katika Kaunti ya Lamu. Serikali iangazie kwa kina shida na matatizo ambayo yanakumba watu wangu. Niko na imani kwamba Serikali ikiamua hakutakuwa na mauaji tena katika Kaunti ya Lamu, hakutakua na mauaji. Tuko na Serikali ambayo iko na uwezo na kila kitu. Kwa hivyo, natoa wito kwa Serikali, hatutaki tena kusikia mauaji ya kiholela katika Kaunti ya Lamu. Vile vile, ningependa Serikali ituambie shida inayosababisha mauaji katika Kaunti ya Lamu. Niko na huzuni na hasira kubwa kwa sababu ya shida na matatizo ambayo watu wangu wanaendelea kupata. Watu wa Lamu ni Wakenya kama wengine. Walindwe kikatiba kwa sababu ni haki yao kulindwa pamoja na mali yao. Asante."
}