GET /api/v0.1/hansard/entries/1370900/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1370900,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1370900/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chute",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13583,
        "legal_name": "Chute Mohamed Said",
        "slug": "chute-mohamed-said"
    },
    "content": "Kwa hivyo, tukienda mapumziko kesho, mimi sijui kama nitaenda Marsabit. Kama watu hao wangepata hizo pesa, wangenunulia familia zao chakula. Watu wetu hawana chakula na wanaendele kuteseka. Sisi tuna shida nyingi sana ingawa tuko katika Serikali moja. Hata ukiwa upande wa Upinzani au Serikali, sisi sote tunahudumia nchi moja, wananchi wetu na familia zetu. Jana Wabunge wa Bunge la Kitaifa walisusia kazi lakini leo wamerudi kwa sababu watalipwa marupurupu yao ya National Government Constituencies Development Fund (NG-CDF). Mimi naona kama hili Bunge la Seneti tunaonyeshwa kwamba halina maana katika nchi hii. Ni mara ngapi Mawaziri wamekataa kuja hapa wakisema wanaugua, mara wako safarini na kadhalika? Lakini wakihitajika kufika mbele ya Bunge la Kitaifa, wanafika. Yamkini siku ya Jumanne, tulihitaji Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Umma kufika mbele ya Kamati ya Uwiano wa Kitaifa ya Seneti, lakini alikosa kuhudhuria. Alisema alikuwa amefika mbele ya Bunge la Kitaifa. Tulipofuatilia, hakuwa ameenda mbele ya Bunge la Kitaifa. Wengine walisema alikuwa Marekani lakini hakuwa huko. Hayo yote ni kuonyesha hawana kazi sana na hili Bunge la Seneti."
}