GET /api/v0.1/hansard/entries/1371028/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1371028,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1371028/?format=api",
    "text_counter": 21,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bwana Spika. Nakaribisha Waakilishi wa Wadi na wafanyikazi kutoka Kaunti ya Embu. Wamekuja hapa kujifunza yale ambayo tunafanya katika Bunge la Seneti. Hapa, tunafanya mambo mengi ikiwemo kutunza ugatuzi. Yangu ni kuwambia wafanye kazi vizuri na waangalie jinsi ambavyo pesa zinatumika huko. Tunapotoa mgao wa pesa kwa kaunti, mfanyie wananchi kazi kule mashinani. Kazi nyingine ya Bunge la Seneti ni kuhakikisha pesa ambazo Serikali kuu inatuma kwa serikali za kaunti inatumika vizuri. Haja yetu ni kuona kwamba ugatuzi haurudi nyuma. Tushirikiane na tufanye kazi pamoja. Mambo mengine ambayo tunaangalia hapa ni kilimo, barabara, afya na kadhalika. Tukiwapatia pesa, mtumie pesa hizo kufanya kazi jinsi inavyofaa, ili mwananchi apate baraka. Mwisho, ni kuwaomba mfanye kazi pamoja na magavana ndio ugatuzi unawiri . Wakati mnataka kuwatimua, muwe mkifanya kazi nzuri ili mkileta gavana hapa, tunamhoji kwa njia inayofaa ndio tusije tukafanya kazi isiyofaa. Kama ni kuhusu pesa au stakabadhi, mkileta gavana hapa, tunajua mambo ya accountability. Hata hivyo, mnatakiwa kwenda kwa Serikali mnapigiwa mhuri ndio tuangalie stakabadhi hizo, kisha msiseme tuko na mapendeleo kwa gavana. Asante."
}