GET /api/v0.1/hansard/entries/1371163/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1371163,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1371163/?format=api",
    "text_counter": 156,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika. Mimi ni Vice-Chairperson wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Naipongeza Kamati yetu kwa kazi tuliyofanya. Tulitemebelea kaunti zifuatazo; Kericho, Kisii, Embu, Kirinyaga na Nyeri. Tulikutana na wakulima ambao wamekuwa wakikuza kahawa kwa miaka mingi. Miaka ya zamani, kahawa ilikuwa mambo yote. Tulipokuwa tunayasikiza maoni ya wakulima, wengi walikuwa na kilio kingi. Walisema kuwa wanalima na kufanya kazi zote na hata kuvuna vizuri lakini wakiuza kahawa, kupata pesa ni shida. Tuliyachukulia maoni yao kwa uzito kwa sababu kahawa ni mojawapo ya mazao ya fedha katika kaunti 35 za nchi yetu. Kahawa ni muhimu ulimwenguni. Kahawa huuzwa Kenya na pia katika nchi zingine za ng’ambo. Tuliposikiliza maoni ya wakulima tuliamua kutafuta suluhisho la kuwasaidia wakulima hao kuweka bei ya mazao yao ili waweze kununua mbolea. Sera"
}