GET /api/v0.1/hansard/entries/1371165/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1371165,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1371165/?format=api",
    "text_counter": 158,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "hizi zitawashawishi wakulima waache kukata miti yao ya kahawa. Ni vizuri turejeshe mambo yalivyokuwa zamani. Kaunti zetu na bodi tofauti zinafanya vizuri kule mashinani. Naaunga mkono Mswada huu na kuomba Seneti izingatie maoni haya ili tuwasaidie wakulima wetu. Revenue collection ya kahawa husaidia serikali na kaunti zote. Hili ni jambo ambalo linafaa kuzingatiwa. Katika kuzingatia swala la kuuza kahawa, tunapendekeza iwe free market na watumie dola za Marekani ili wakulima wapate pesa zao kwa haraka. Mambo mengine ambayo tuliangazia yanahusu masaibu dhidi ya mkulima na serikali inayouza kahawa kwa nchi za ng’ambo. Kuna c artels zilizoko pale. Ninaomba n ational Government andcounty governments ziangazie mambo haya ili mkulima asinyanyaswe na apate pesa za kuisaidia familia yake. Tukiyatimiza mapendekezo haya, mkulima ataweza kujikimu na familia yake na vile vile kumudu huduma za afya. Kwa sababu kahawa ni kila kitu kwa wakulima wa kahawa, wanapaswa kupatiwa mbolea. Baada ya kuvuna na kuuza mazao yao, wakulima hao wataweza kulipa deni. Nashukuru Serikali kwa kutenga Kshs4 bilioni ambayo imesababisha kupungua kwa bei ya mbegu ya kahawa hadi Ksh100."
}