GET /api/v0.1/hansard/entries/1371901/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1371901,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1371901/?format=api",
    "text_counter": 268,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili nichangie mjadala huu kutoka kwa Sen. Crystal Asige. Tumeyasikia mambo ya mauaji mara kadhaa kwa miaka na siku nyingi. Katika Bibilia uuaji umekataliwa. Tumeyasikia kutoka kwa vijana, wazee na akina mama. Mambo haya yanachangiwa mara mingi pia katika boma zetu. Naomba tuyakomeshe mambo haya kwa kutengeneza sheria zitakazotuonyesha kuyafuatilia mambo haya. Vijana wote wameadhirika. Wanakosana kuhusu vyama, pesa au mapenzi. Nini kitakacho tumika kukomesha mambo haya? Watu wanapokosana nyumbani- bibi na bwana wanapigana na kuuana. Katika shule zetu za sekondari na vyuo kikuu, unapata vita vinaibuka vijana wanapokataliwa na wasichana. Pia imechangiwa na tunavyokaa na uongo mwingi. Ningewaomba watoto wetu walio shule wajue ni akina nani wanaotemeba nao. Unaweza kuwa unatembea na rafiki na kumbe ni adui yako. Ningeomba tupate suluhisho ili mambo haya yasifanyike tena. Inaweza kuibuka kutokana na biashara. Mambo haya yanaleta shida kubwa. Naomba vijana ikiwa msichana amekukataa haina haja ya kumuua kwa sababu utapelekwa jela. Wasichana pia watazame wanaotunga urafiki nao kwa sababu uongo ni mwingi. Ningeomba tutafute kinacholeta tashwishi ili tutembee pamoja. Mwisho, Serikali inafaa kuingilia mambo inayowahusu watoto wa shule; madawa ya kulevya kama bhangi na kadhalika. Naomba mambo haya yaangaliwe vizuri ili tusiyasikie mambo ya mauaji tena. Tunafaa kutembea pamoja kama Wakenya. Katika Biblia hakuna maneno ya wanaume au wanawake. Sote mbele ya Mwenyezi Mungi ni kitu kimoja. Naunga mkono."
}