GET /api/v0.1/hansard/entries/1371903/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1371903,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1371903/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13733,
"legal_name": "Agnes Kavindu Muthama",
"slug": "agnes-kavindu-muthama"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili nichangie mjadala huu wa kudhulumiwa na kuuawa kwa wanawake pamoja na watu kukosa haki yao. Ninaongea na uchungu mwingi sana moyoni kwa sababu katika Kaunti ya Machakos nimewapoteza several ladies - wasichana na kina mama kadhaa kupitia haya mauaji ya kiholela. Juzi, tumempoteza Rita Waeni Muendo. Ametoka Kaunti ya Machakos na aliuawa kinyama sana. Alikatwa miguu na pia kichwa chake kilipatikana kwingineko. Ni lazima wasichana wetu wajichunge. Wajue wanatembea na akina nani na ni watu wa aina gani. Mambo yanayochangia sana wasichana wetu kuenda na kupatana na madhara ya aina hii ni ukosefu wa ajira. Wengi wamekosa kazi na kutembea kiholela kwa sababu ya"
}