GET /api/v0.1/hansard/entries/1371905/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1371905,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1371905/?format=api",
"text_counter": 272,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13733,
"legal_name": "Agnes Kavindu Muthama",
"slug": "agnes-kavindu-muthama"
},
"content": "shida, taabu na dhiki wanazopitia. Ni lazima tuwachunge wasichana wetu vizuri. Tuwapatie kazi kama Serikali ili wajidumu kimaisha na kuepuka mipango kama hii. Tumeona pia hata nyumbani wanawake wakichinjwa kama mbuzi. Sio kwamba ni wao wanauawa tu lakini zaidi yao ni wanawake ambao wanauawa kiholela. Kwa sababu mtu ana wivu anachinja mtu bila sababu. Hakuna aliye na ruhusa ya kutoa mwingine uhai katika sheria na pia Biblia. Hakuna mtu aliye na maisha ya kumpa mwingine. Naomba hatua kali zichukuliwe kwa waliowaua wale wasichana, Juzi, nilisema kuwa Serikali ina mkono mrefu sana. Ikitaka ku arrest wale watu, itafanya vile na wafungwe ili iwe funzo kwa hao na wengine wote. Si mambo ya mauaji tu. Utapata dhuluma za kiboma ni nyingi sana. Utapata mama yuko pale nyumbani lakini zile dhuluma na shida anazozipitia ni za ajabu kwa sababu ni mwanamke. Utapata baba ako na ruhusa hata ya kuuza ng’ombe lakini mama hana ruhusa ya kuuza hata kuku. Hiyo inakuwa ni dhuluma ambazo sio nzuri. Sen. Crystal Asige, ningeomba ukiangalia hii law, angalia pia law ya marriage na"
}