GET /api/v0.1/hansard/entries/1371923/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1371923,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1371923/?format=api",
"text_counter": 290,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia katika Hoja ya dada yangu. Pia, niweze kuomboleza na taifa ya Kenya kwa kupoteza watoto wetu wa kike; akina mama ambao wameolewa katika ndoa zao na wasichana ambao wamepoteza maisha yao. Asilimia 39 hadi 47 ya wanawake ulimwenguni wanaishi katika ndoa ambazo wananyanyaswa. Asilimia 70 ya wanawake ulimwenguni wamekuwa wakiuliwa kwa sababu wao ni wa jinsia ya kike. Takwimu zinaashiria ya kuwa idadi kubwa ya wale ambao wametuacha kwa mauaji haya ya dhuluma, wameuliwa kwa sababu waliingia katika mahusiano na watu ambao waliwapenda tu kama wanawake; jinsi maumbile yetu kama wanawake, Mwenyezi Mungu alitubariki, ili tuweze kupeana mapenzi. Lakini mwishowe wanawake wanadhulumiwa. Naongea na taifa la Kenya kama kiongozi wa kike kwenye Bunge la Seneti. Nawaomba wazazi na jamii kwa jumla isisukume watoto wa kike katika mahusiano. Kama mtoto wa kike hajakuwa tayari kuolewa, tuwache tabia ya kila tunapokutana katika jamii, kuwapa msukumo waingie katika mahusiano. Changamoto hii inawapata watoto wa kike ambao wamesoma, wamejiweka katika maisha vizuri lakini imekuwa ni lazima watu wafuate mkumbo. Kufuata mkumbo ni kwamba tumewekewa kiwango cha miaka ambacho tukikifikisha sisi kama watoto wa kike hata kama hatujapata kipenda roho, ni lazima tuonyeshe jamii kwamba tumeolewa. Bw. Spika wa Muda, naomba leo kuzungumza na akina mama ambao wanaishi katika ndoa ambazo wananyanyaswa. Wasiogope kunyoshewa kidole cha lawama ati kwa sababu wamejikwamua kutoka yale mateso ambayo wanaendelea kuyapata. Sisi kama taifa tumelifanya jambo la kawaida mtoto wa kike anaporudi nyumbani kupeana malalamishi kuhusu yale mambo ambayo anapitia katika ndoa yake, tunambebesha virago na kumwambia huyu ndiye ulituletea kwa hivyo nenda ukamalize safari na mwenzako. Tunaishi katika ulimwengu tofauti na ule wazazi wetu waliishi. Tunaishi katika ulimwengu ambao msongo wa mawazo unaumiza watu. Tunaishi katika jamii ambayo mtoto wa kike amewezeshwa kiasi cha kwamba akiwa yeye ndiye mtafutaji katika jamii, mtoto wa kiume hataki kukubali kwamba huyu mtoto wa kike anaweze kuenda kazini na arudi awezeshe jamii yake. Bw. Spika wa Muda, langu kwa dada zangu wa kike wa umri wangu na wale ambao wamenizidi ni kuwaomba wasilazimishe mahusiano ikiwa hauko tayari, wala usikubali kupelekwa na shengesha ya vitu ambavyo unaviona katika Social Media . Hakuna kitu kama perfect life, marriage na relationship . Nawaomba mchukue muda wenu mwafaka mnapochagua mtu ambaye mtaendelea kuishi naye katika maisha yenu. Iwe in mtu ambaye umempenda na uko tayari kufa kuzikana kukaa naye na siyo yeye akulazimishe kuenda jongomeo naye akibaki nyuma kutafuta mrembo mwingine. Nawashukuru viongozi wote wa kiume ambao wamebaki hapa ndani ilikuwezesha kupaza sauti za mtoto wa kike katika jamii hii. Sisi ni warembo, mtupende,"
}