GET /api/v0.1/hansard/entries/1371930/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1371930,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1371930/?format=api",
    "text_counter": 297,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 380,
        "legal_name": "Shakila Abdalla",
        "slug": "shakila-abdalla"
    },
    "content": ", lakini, tunaseme anayekukumbuka ni binadamu. Kwa hivyo, tunasema asante kwa Sen. Munyi Mundigi. Pia, ningependa kusema ni kwamba hakuna mwanamke ama binadamu anayestahili kufa kwa sababu ya mapenzi. Kifo kimepangiwa muda wake na sababu zake. Lakini sababu ya mapenzi haistahili mtu kupoteza maisha yake. Bw. Spika wa Muda, mwanamke ama binadamu yeyote anayepoteza maisha, kitu cha muhimu ni haki ipatikane kwa kufuata sheria. Bw. Spika wa Muda, katika nchi yetu ya Kenya hatuna shida ya sheria. Sheria za Kenya ziko nyingi sana ambazo kwamba zinampatia kila mtu haki kikamilifu. Shida ni kwamba utekelezaji wa sheria ndio changamoto kubwa katika nchi yetu. Kwa hivyo, dhuluma za kijinsia zinasababishwa na kukosa kutekelezwa kwa sheria zinazoambatana na hizo dhuluma. Bw. Spika wa Muda, hatuko hapa leo kusema kwamba tulikuwa na shida hii, wamama hawa wameuawa, kupeana ripoti ama kupeana hesabu. Tuko hapa kutaka suluhisho ya hii shida ambayo inazidi kuendelea na suluhisho halijapatikana. Bw. Spika wa Muda, dhuluma kama hizi zikifanyika, kwa mfano kama ni hoteli, inafaa ifungwe na polisi waende wachukue rekodi za wale ambao waliweka nafasi katika hoteli hiyo wakaacha vitambulisho vyao na majina yao kamili. Ni rahisi sana watu kama hawa kushikwa. Tunashindwa ni kwa nini Serikali na sheria imezembea katika kupambana na magaidi kama hawa wanaoenda wakiuwa wasichana wa wenyewe na wamama kiholela. Kwa hivyo, kama sheria ingechukuliwa, hoteli hizo zingekuwa zimefungwa na watu kuchukuliwa vibali vyao, kuchunguzwa, kusororwa na kujulikana ni kina nani wauwaji, bila shaka, haya mambo yangekoma. Kwa kuwa sheria haitekelezwi, mambo hayo yanazidi kutendeka. Dhuluma za kijinsia hazitakoma kwa sababu unyanyasaji uko ndani, nje, juu na chini. Hayo yote yanachangiwa na watekelezaji wa sheria ambao hawawajibiki na kuchukua hatua mambo hayo yakifanyika. Bw. Spika wa Muda, ningependa kusisitiza kwamba sheria zinafaa kutekelezwa kikamilifu ili haki ipatikane kwa wasichana wanaoumia."
}