GET /api/v0.1/hansard/entries/1371933/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1371933,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1371933/?format=api",
    "text_counter": 300,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cherarkey",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13217,
        "legal_name": "Cherarkey K Samson",
        "slug": "cherarkey-k-samson"
    },
    "content": "sababu ya vita vya kijinsia. Kuna kesi iliyoamulia juzi kuhusu suala hili, ambapo marehemu Monica Kimani aliuawa kwa njia isiyo eleweka. Mahakama imetoa hukumu kuhusu kesi hiyo. Inamaanisha kuwa kuna sheria za kutosha za kupambana na janga hili. Jambo la kushtua ni kwamba mara nyingi asasi za usalama nchini Kenya hazizingatii vita vya kijinsia kama janga linaloathiri jamii zetu. Wanaume wengi katika taifa la Kenya wanaheshimu akina mama. Ni wachache tu ambao wana unyama. Nakubaliana na wenzangu waliosema kuwa vyumba vya raha na starehe ambavyo vinatumika kama hoteli na mikahawa vinafaa kusajiliwa na Wizara ya Masuala ya Ndani na Utawala ili tujue nani wanaingia huko na saa ngapi. Tukifanya hivyo, itakuwa rahisi sana kufuatilia mauaji kama yale tunayoshuhudia dhidi ya kina mama na wasichana. Ikiwa tutafanya hivyo kama taifa, tutajaribu kuzuia mauaji yanayotokea kiholelaholela. Jambo la pili ni kuwa tuna jukumu kama taifa kubadilisha taasubi katika jamii zetu mbalimbali. Wanawake kwa wanaume wote ni sawa kwa njia mbalimbali. Mungu anajua kwa nini wengine ni wa kike na wengine ni wa kiume. Naomba wanaume wa Kenya ambao wana tabia hiyo wakome. Wasipokoma, sheria itachukuliwa mara moja. Hakuna haja ya kumpiga mtu ngumi ama kofi kwa sababu sisi sote ni binadamu. Wanaume wajue kwamba mwanamke anafaa kupigwa na kanga ama leso bali si kushambuliwa kwa makonde na ngumi. Mwanamke vile vile anafaa kupendwa kwa kupewa pesa. Hayo ndiyo mapenzi. Watu wa jinsia ya kike, hasa wasichana, wanafaa kuacha kula nauli ya wanaume kwa sababu ni changamoto hasa kwa vijana ambao wanajaribu kujikimu. Bw. Spika wa Muda, ukiniruhusu kutumia lugha ya mtaani, wanasema “kula fare”. Hiyo ndio changamoto. Hata hivyo, hiyo haifai kuwa sababu ya kumuumiza msichana ama mvulana kwa njia yoyote. Ningependa Maseneta wenzangu wafahamu kwamba hili si jambo ambalo linaathiri jinsia ya kike pekee. Kuna wavulana wengi ambao huumizwa roho na kuamua kujinyonga kwa sababu ya mapenzi au kukataliwa na wasichana. Ijulikane kwamba wao pia ni binadamu na wana malengo fulani. Ninauliza akina mama na wasichana, iwapo humpendi mvulana au mzee, mwambie mapema awache kukununulia kahawa, vikaukau na vipanzi. Pia, awache kukuburudisha na kukupeleka kwa nyumba za starehe. Ikiwa tutakuwa na heshima ya mapenzi, nafikiri kama taifa, tutakuwa mbele. Bw. Spika wa Muda, la mwisho kwa maana naona masaa yameyoyoma, ni kwamba, ningependa kumwuliza Sen. Crystal Asige apendekeze jambo lolote ambalo litaweza kubadilisha sheria yeyote katika Bunge hili. Sisi kama Seneti tutasimama, tubadilishe sheria ya kuchunga wavulana kwa wasichana, kwa sababu hilo ndilo lengo letu. Wakati tunaposherehekea siku ya wapendanao, ingekuwa vizuri kukumbuka wale wamama ambao wameumizwa na wanaume hao. Asante sana kwa kunipa fursa hii."
}