GET /api/v0.1/hansard/entries/1371942/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1371942,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1371942/?format=api",
    "text_counter": 309,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa nafasi hii. Leo watu wanasherehekea mapenzi lakini inategemea ni mapenzi ya nini. Kuna wale wanapenda pesa, mvinyo, chakula na mavazi, na yote ni mapenzi. Nataraji kwamba hicho ndicho kiini cha mjadala wa siku ya leo. Kuna wale wana mazoea ya kuvuna wasipopanda, wale ambao hutabasamu vilivyo tayari pasipo kushughulikia kuviandaa na wale walio tayari kupakua na sio kutafuta kuni kuandaa. Donda hili ndilo linalotusumbua sisi kama jamii. Wale ambao wanaomiliki maeneo ya starehe na kujivinjari, na maeneo haya ya Airbnb na kadhalika, ni lazima tujue ni wapi ama ni sheria zipi zinadhibiti kuchipuka kwa maeneo haya ya burudani. Bw. Spika wa Muda, wengi ambao wamehusika katika mauaji ni watalii ama wageni kutoka nchi tofauti. Ni lazima vile vile Serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Maswala ya Ndani kudhibiti wanaokuja au kuzuru nchi hii ili wasije wakaleta tabia au hulka ambazo hazieleweki, ili kwamba kuweka wanawake wetu katika hali tatanishi. Rafiki yangu mmoja aliniambia lile linalowakumba vijana wengi, wasichana kwa wavulana, ni kuhisi kujikuna lakini hawajui watajikuna vipi. Wanatarajia kula lakini hawajui watauma vipi. Ni lazima jamii na haswa, viongozi wanawake humu nchini Kenya--- Iwapo tungekuwa tunajadili mambo ya tabia na tamaduni nzuri; na mambo ya kulinda na kukuza wasichana wetu katika njia nzuri kutoka Januari hadi Disemba, siku ya leo ya mapenzi hatungevaa nguo nyeusi. Bw. Spika wa Muda, sababu baadhi ya wale wanatajika nchi hii katika vyombo vya habari na maisha yao ni kinyume na familia zinazoheshimika, familia ya bwana na bibi wanaopendana. Wao hutamka tofauti. Lakini leo wanadai watu waheshimiwe. Heshima ya umenge au jinsia hudhibitishwa ama hukuzwa kutoka nyumbani. Ninaomba viongozi, Maseneta, Wabunge na Mawaziri waanze kukuza na kufunza wasichana wetu kwamba hakuna cha bure duniani. Zile hoteli nzuri ambazo wanaingia wakitabasamu wakaangalia paa, watu wametolea jasho. Vile vyakula vinavyoandaliwa wakila wakiwacha, watu wametolea jasho. Ni lazima wajiulize kile unachopata bure, anayekupa anatafuta nini. Siye yule anatabasamu akikutazama anakupenda kwa haki. Ni kama fisi ama simba anavyomwona mwanakondoo. Kondoo anadhani simba ana manyoya, amefurahia. Hapana, simba anamwonea huruma tu. Lazima jamii ya Kenya tuketi kujadili mambo haya kwa kina. Viongozi wa makanisa kando na kuhubiri mbinguni, ufalme upo hapa. Tunataka kuzungumza na wazee, kina mama na vijana. Tuelewe kwamba ni lazima tuishi pamoja kwa kuelewana. Mapenzi ni ya roho safi kama Yesu alivyohubiri. Ila isiwe ya siku moja kama ya leo tunavaa nguo nyeusi, tunalalamika na kufunga ukurasa. Je, kesho? Tuweke mikakati, idara ya elimu, makanisa na serikali tuje sote pamoja kwa sababu hili ni jambo ambalo linatuathiri sisi wote kutoka nyumbani kwetu hadi taifa. Nakashifu mauaji ya wanawake, uporaji wa pesa za wanaume, ulaji wa rasilmali ovyo ovyo. Cha muhimu ni tuishi pamoja, tupendane. Nipe nikupe patashika katika Maisha."
}