GET /api/v0.1/hansard/entries/1372075/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1372075,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372075/?format=api",
    "text_counter": 120,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika kwa nafasi hii. Vile vile, ningependa kuongenza sauti na mchango wangu kwa mchakato wa muda utakao chukua Rais kuhutubia jamii ya Kenya na vile vile sisi kama viongozi wajumbe katika Seneti, kutoa michango yetu. Isiwe ni kwamba, Rais anapohutubia nchi katika jumba la Kitaifa, kuwe na sherehe za kitaifa, pale ambapo anazungumza, tunapiga makofi, watu wanakunya na kula na kuhesabu siku baada ya siku. Tunataraji kwamba, yale ambayo viongozi katika jumba hili watatamka, mikakati ama vile mdahalo utakvyo kuwa unachukuwa mikondo tofauti, lazima mawaziri ambao watakuwa wameambatana na Rais wahakikishe kwamba mabadiliko haya yanashuhudiwa katika wakati unaostahili. Bw. Spika, sisi ambao tuko katika Serikali, tunajukumu kubwa kwamba, ijapokuwa tunawapa watu matumaini lazima washuhudie na wajihusishe katika kutekeleza yale tunazungumza. Najiunga na wale katika mrengo wa upinzani kwamba, isiwe Rais akizungumza, ni kana kwamba ametamatisha yale yote atakayo sema ama atakayo fanya, lakini ni kuhakiksha ya kwamba, anapozungumza, atende. Kutenda kwake ni sisi katika Serikali kuhakikisha kwamba tunasukuma mawaziri kutekeleza yale ambayo tunataka."
}