GET /api/v0.1/hansard/entries/1372077/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1372077,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372077/?format=api",
    "text_counter": 122,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Bw. Spika, mwaka wa 2027, tutakuwa katika mchakato wa kura na wapiga kura watatuuliza mlizungumza, mkatupa matumaini lakini hamkutenda chochote. Mimi kama mkereketo wa Serikali ningetaka Rais aje na ikiwezekana, aje katika Jumba la Seneti, sababu Seneti huzungumza mambo ya kaunti. Kuna pesa ambazo wanabiashara hawajalipwa na kuna mikakati au ajenda za kaunti ambazo sisi hujadili. Ni lazima Rais ajue kwamba yale tunayotarajiwa kufanya kama Seneti ni tofauti sana na yale ambayo wale walio katika Jumba la Kitaifa hufanya. Anapopeana mwelekeo kuhusiana ugatuzi, ni lazima Wakenya wajue Jumba la Seneti ndilo ulinzi, matumaini au ngao ya ugatuzi katika nchi ya Kenya. Bw. Spika, mimi naunga mkono tupewe nafasi mwafaka tujieleze na Rais pia atusikize ndio baadae yeye au Mawaziri wake watekeleze yale ambayo tunazungumza hapa. Siamini kwamba Seneta yeyote katika nchi ya Kenya anaweza amka hapa akapeana mwelekeo hafifu ama akapotosha Rais kuhusiana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na falsafa ya nchi. Ni lazima atusikize sisi wote na atende kwa mujibu wa Katiba. Asante sana."
}