GET /api/v0.1/hansard/entries/1372099/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1372099,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372099/?format=api",
    "text_counter": 144,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika naunga mkono yale mambo tunayo yazungumzia hapa. Tumekubaliana muda upunguzwe ili kila Seneta kati yetu sote 67 apate nafasi ya kuchangia. Tunatoka mashinani na tunajua vile kulivyo. Naunga mkono kwa sababu nakumbuka mwaka jana Rais alipolihutubia Bunge, alizungumza mambo mengi kuhusu uchumi, afya mashinani na hilo tumeona ametimiza. Vile vile, aliongea kuhusu kilimo na tunaona vile mambo yanaendelea. Tulichangia na kumuunga mkono kwamba tutakuwa tunachangia tuone kama kuna mambo yanaweza kubadilika. Wakati huo, macadamia yalikuwa yanauzwa kwa shilingi 30 na kwa sasa ni shilingi zaidi ya 100. Kwa hivyo, kuchangia hotuba ya Rais ni jambo muhimu sana. Rais pia alizungumzia swala la kilimo na mbolea - ikashuka kutoka shilingi 5,500 hadi shilingi 2,500. Hivyo basi tumeona vile kilimo kinaendelea na mambo mengine mengi. Hivyo basi, ni vyema muda upunguzwe ili tuwe tunachangia mambo mengi. Ningependekeza pia tuwe tunachangia vile tutatilia maanani mambo ya kilimo ili kila kaunti iwe inapata maji ya kulima na vinginevyo ndio tuimarishe mazao mazuri. Tukichangia haya yote, mambo ya pesa mkononi itarudi. Vilevile Rais aliangazia hali ya uchumi. Ni kweli tumeona kumekuwa na shida. Alieleza vile madeni yamekuwa mengi na vile amekuwa akiyalipa na kusaidia kaunti. Hivyo basi, tumeona kaunti nyingi zikipokea pesa kila mwezi kuanzia mwezi wa saba mwaka uliopita kinyume na miaka ya hapo awali. Tungetaka pia kuchangia kuhusu vijana wetu ambao wametelekezwa. Hivyo basi, kwa sababu ya uraibu wa pombe na madawa ya kulevya, itafika wakati ambapo Kenya itakuwa haina vijana na familia. Kuna haja basi tuone kama kila kaunti inaweza kupewa pesa ili ipeleke kwa hawa vijana kwa mafunzo. Hii itawaepusha na vileo na wataweza kukaa vizuri na familia zao. Asante Bw. Spika, na naunga mkono."
}