GET /api/v0.1/hansard/entries/1372107/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1372107,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372107/?format=api",
    "text_counter": 152,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "(CBC). Sisi kama viongozi wachanga, ambao ndio sasa tunaanza ulezi, tuko na watoto wetu katika taasisi hii. Watoto wetu wameanza kusoma na mpaka sasa hakuna mwelekeo wa kuonyesha watoto hawa watakwenda vipi. Japo wengine wetu tunasemekana kwamba ni vibaraka wa Serikali, nawakumbusha Wajumbe wenzangu hapa mimi ni Mjumbe wa kike niliyepewa fursa kuja katika Bunge hili kuongelea maswala ya kijinsia na kuwasaidia kuongeza na kutilia pondo pale ninapoona kuna sheria zinatungwa na zinatuumiza sisi kama kina mama, ama nichangie kuonyesha njia mwafaka ya kufuata itakayosaidia kina mama na vijana katika taifa hili la Kenya. Nataka kuwaambia ndugu zangu ambao wakienda mashinani wanasema kwamba Wajumbe wa upinzani hawapewi fursa sawa na Wajumbe walioko upande wa Serikali kutunga sheria; huo ni uwongo wa mchana. Hapa kila mtu ako na fursa ya kutunga sheria na kuchangia hisia zake ili kuleta suluhu katika taifa la Kenya. Tuko hapa ili kuwasaidia Wakenya ---"
}