GET /api/v0.1/hansard/entries/1372129/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1372129,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372129/?format=api",
"text_counter": 174,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipatia fursa hii kuchangia Hoja ya kuweka muda katika kujadili Hotuba ya Rais ambayo inatarajiwa mwezi wa nne. Kwanza, ninachukua fursa hii kukutakia wewe binafsi na masenata wote mwaka mpya wa elfu mbili na ishirini na nne wenye manufaa na afya njema. Pili, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba ametufikisha mwaka mpya na tuko tayari kufanya kazi katika kujenga taifa na kuhakikisha ya kwamba maisha ya wakenya yamebadilika. Hoja hii ni muhimu sana kwa sababu, tumeona kwamba mwaka uliyokwisha, watu wengi hawakupata fursa ya kuchangia Hotuba ya Rais na Hotuba ile ilikuwa na mambo mengi ambayo ni kinyume na hali halisi ilivyo katika inchi yetu ya Kenya. Ni kweli kwamba wengi wetu huwa tunaikosoa Hotuba hii na kwa kweli hiyo ndiyo kazi yetu kwa sababu, sisi tumechaguliwa kama wawakilishi wa wanainchi. Sisi ndio macho ya wananchi, na ikiwa kuna jambo ambalo limezungumzwa ama limefanywa ambalo halilingani na sheria, ama halilingani na hali halisi ilivyo, ni wajibu wetu kulikozoa na kueleza ukweli halisi ulivyo tukipata fursa ya kukozoa Hotuba hii. wengi wetu ambao wako katika upande wa serikali wanajiona kuwa wao ni serikali zaidi ya wale ambao wako katika Mkono wa Serikali, the Executive. Lakini, tukiangalia majukumu yetu katika Katiba, kifungu cha tisini na sita ni kwamba, sisi ni macho ya wanainchi katika Serikal na mbali na ya kwamba tunatunga sharia na kukozoa serikali, pia sisi ndio waangalizi wa mali ya uma katika mikono ya serikal ambayo wananchi hawawezi kufanya hivyo. Kwa hivyo, mimi nina unga mkono Hoja hii na ningependa kukomea hapo."
}