GET /api/v0.1/hansard/entries/1372213/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1372213,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372213/?format=api",
"text_counter": 258,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kwanza, najiunga na wenzangu ambao wametangulia na kupinga marekebisho haya. Hii ni kwa sababu maji ni haki ya kimsingi ya kila mwanadamu. Sisi kama Wakenya, hii ni kati ya haki zetu za kimsingi. Mswada huu unajaribu kufanya maji iwe kama biashara. Hii itasababisha wananchi wa Kenya kukosa maji na kupata taabu ya kupata maji. Tukiangalia mfumo wa sasa, kule pwani, kuna Coast Water Services inayomilikiwa na Serikali Kuu. Kuna shirika ambalo linauza maji katika kila kaunti. Kwa mfano, la Mombasa ni Mombasa Water and Sewerage Services. Linanunua maji kutoka kwa Coast Water Services halafu linawauzia watu wa Mombasa. Iwapo huu Mswada utapita, ina maana kwamba, Coast Water Services Board itakuwa na uhuru wa kuuza maji kwa mtu binafsi ama shirika la kibinafsi, halafu wale watakuja kuwauzia watu kwa bei ya juu. Bw. Naibu Spika, asilimia kubwa ya wakaazi wa Mombasa hawapati maji. Hii ni kwa sababu, maji yenyewe yanayotoka kwa Chemi Chemi ya Tsavo ni yatoshi na pia yale yanayotoka Malindi hayatoshi. Haikimu mahitaji ya watu wa Mombasa. Iwapo Mswada huu utapita, utatoa nafasi kubwa kwa wawekezaji wa kibinafsi kuuza maji kwa bei ya juu. Kwa vile maji ni kitu cha muhimu kwa maisha ya binadamu, hiyo itakuwa na kinyume na usalama wa nchi. Wananchi wakikosa maji, yataathiri usalama wao na wa nchi kwa jumla. Jambo la pili ni kuna shirika ambalo linaitwa Water Storage Authority . Kwa sasa, hakuna sehemu ambayo hupata maji kwa masaa 24, siku saba kwa wiki katika kaunti zote. Hata Murang’a Kaunti pia wanachangamoto za kutekeleza hilo. Kwa hivyo, tunaunda shirika la kuhifadhi maji. Litakuwa na kazi gani? Kwa mfano, kule pwani, Chemi Chemi ya Tsavo imekuwa na pipe moja kutoka 1945 ilipoanzishwa, hadi sasa 2024. Serikali imeshindwa kuweka hata pipe moja kutoka Tsavo kuja hadi Voi, Mombasa ama Kilifi. Bw. Naibu Spika, ukiangalia makazi yalivyokuwa kule 1945 siyo kama yalivyo leo. Hii ni kwa sababu kuna miji kadhaa imekuwa kuanzia pale Mtindo Andei. Hii ni kwa sababu Chemi Chemi ya Mzima Springs iko nyuma ya Mtito Andei. Kwa hivyo, kutoka hapo kwa hiyo barabara mpaka Mombasa, kuna miji mingi ambayo imekuwa kutoka 1945 hadi wa leo. Wote hawa, wanategemea pipe moja ya Mzima Springs."
}