GET /api/v0.1/hansard/entries/1372384/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1372384,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372384/?format=api",
"text_counter": 115,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana. Mhe. Spika. Na mimi kama Mama Mombasa nachukua fursa hii kutoa rambirambi zangu za pole pamoja na wakaazi wa Mombasa kwa familia ya Kelvin Kiptum. Alikuwa ni shujaa na kijana mahiri katika mbio. Ningependa pole zangu zimfikie baba yake ambaye alilia sana kwa uchungu akisema ni mtoto wake wa kipekee. Alisema kuwa watu asiyewafahamu walienda kwake na kujitambulisha kuwa walitumwa kutoka sehemu fulani. Napiga pondo nikisema hili jambo lichunguzwe pengine kuna mkono wa mtu. Ningependa kuwakumbuka pia na mabinti wetu ambao wameuliwa hivi karibuni. Natoa rambirambi zangu kwa familia zao. Naiomba Serikali iangalie vifo hivi vinavyotokea maana ni vya kusikitisha sana. Ahsante sana, Mhe Spika."
}