GET /api/v0.1/hansard/entries/1372451/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1372451,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372451/?format=api",
    "text_counter": 23,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, mimi ni Sen. Munyi Mundigi, Seneta wa Kaunti ya Embu. Ningependa kuchangia kuhusu mambo ya mashamba. Najua mambo ya Muthanthara kidogo. Kuna sehemu inaitwa Igambang’ombe ingawa sikuwa najua mambo haya kabisa. Ninavyojua, kuna watu wanaoishi Muthanthara. Mara nyingi huwa kuna matatizo Serikali inapotoa pesa kwa sababu watu wa Kaunti ya Tharaka-Nithi huwa wanasema huko ni kwao. Wengine wanapiga kura huko na wengine wanapiga kura upande wa Mbeere ambayo iko katika Kaunti ya Embu. Mara nyingi huwa kuna shida kuhusu maji au jinsi county government inavyofanya kazi. Ni vizuri viongozi wa kaunti hizo mbili waketi chini ili kuangalia jinsi watu hao wanaweza kusaidiwa, ili waishi maisha mazuri. Wanafunzi wanafaa kwenda shuleni bila matatizo na wenyeji wapate hati za mashamba . Kwa kuwa jambo hilo limeletwa katika Seneti, ni vyema tuliangazie kiundani ili kupata suluhu. Tunafaa kujua kama watu hao wako katika Kaunti ya Embu ama Mbeere na pia wapate title deeds zao kama wengine. Kwa hivyo, naunga mkono Ardhi hali hii ili watu hao waweze kupata haki yao na tujue ukweli. Viongozi wa kaunti hizo mbili wanafaa kuketi chini na kuelewana kuhusu mambo ya mashamba. Kuna watu wamejenga nyumba za mawe. Vile vile, kuna kanisa na shule. Sehemu itakayobakia, watu wapewe kidogo kidogo ili kila mtu apate."
}