GET /api/v0.1/hansard/entries/1372462/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1372462,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372462/?format=api",
"text_counter": 34,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13592,
"legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
"slug": "onyonka-richard-momoima"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda. Kila wakati Sen. Cherarkey anapozungumza siasa anamkumbuka Mzee Raila Odinga. Sijui kama akiwa kitandani na bibiye pia Mzee Raila huingia pale kati kati kumsumbua na kuharibu hewa yake. Kwa kinaga ubaga, swala la ardhi ni jambo ambalo limeletwa katika Bunge hili la Seneti. Zamani nilifikiri kuwa maswala haya huyasumbua wakaaji wa Pwani, watu wa eneo la Bonde la Ufa au wakaazi wa Kaunti ya Nairobi City. Shida tunayo nchini kwetu ni kuhusu swala hili la ardhi. Lazima kama Bunge la Seneti tujipange na tuhakikishe tunatumia kamati husika na kuhakikisha suluhisho la kudumu limetafutwa ili tumalize shida hizi za ardhi nchini. Bw. Spika wa Muda, ugumu umeingia haswa baada kwa Mheshimiwa Rais William Ruto alipoleta ratiba ya kujengwa kwa nyumba katika maeneo wakilishi ndani ya kaunti zote nchini. Eneo la Trans Nzoia ni mojawapo ya maeneo yaliyo kwenye Bonde la Ufa. Juzi kulikuwa na matangazo kuwa Rais alielekeza waliyo na shamba zilizokuwa za serikali zamani na zilizokuwa zimesimamiwa na Idara ya Jela zirudishwe ili zithibitiwe na Serikali. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}