GET /api/v0.1/hansard/entries/1372463/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1372463,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372463/?format=api",
    "text_counter": 35,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13592,
        "legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
        "slug": "onyonka-richard-momoima"
    },
    "content": "Katika Kaunti ya Kiambu, hususan eneo la Thika, kuna shida inayohusu shamba la Del Monte. Hadi sasa hakuna jawabu. Tukirudi katika Bonde la Ufa, Sen. Cherarkey na wenzetu wamefanya kazi nzuri sana. Wakaazi wa Kaunti ya Kericho pamoja na kampuni za ukuuzaji chai wanazungumzia swala la ardhi. Bw. Spika wa Muda unatoka eneo hili na nimeona ukiyashughulikia mambo haya. Nawasihi waliyo na fursa ya kuongea na Rais pamoja na Mawaziri wanao kushughulika na mambo ya ardhi, watupe ruhusa ya kuangalia maswala ya ardhi na migogoro ambayo imetokea ili kama viongozi, Rais wa nchi yetu na wahusika wote tujaribu kupata suluhisho kwa heshima, haki na kisheria. Hili ndilo jambo ambalo ningetaka kuuliza ndugu zangu ambao wako hapa. Ingewezekana, Seneti ingejaribu kutatua mizozo ya ardhi katika nchi hii. Tuichukue kamati na tujihusishe ili tutafute suluhisho. Ukiona vile Wakenya wanafurushwa kutoka makaazi yao, wanaambiwa court"
}