GET /api/v0.1/hansard/entries/1372467/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1372467,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372467/?format=api",
    "text_counter": 39,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13592,
        "legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
        "slug": "onyonka-richard-momoima"
    },
    "content": "ya kuwazuia kubomoa nyumba imetekelezwa. Haya mambo yote yatafanya wananchi na wageni ambao wangependa kuleta hela zao ili wakuze rasilimali ya nchi yetu wadidimie kama hatutapata suluhisho kuhusu mambo haya. Kwa kingereza tunasema the Land question in Kenya must be sorted out for us to continue movingeffectively as a country. Tuwe nchi ambayo ina heshima, inafuata sheria na ambayo inampa mwekezaji nafasi ya kuweka mali yake, ajue kuwa wanaweka pesa mahali ambapo sheria inafuatiliwa na hamna shida ya ardhi. Bw. Spika wa Muda, tunapojadili na kuyaangalia haya maswala, Bw. Spika wa Muda umesafiri na kutazama nchi ya Rwanda. Wakenya ndio walitengeneza mikakati hiyo. Ukiwa kule unaweza pata nambari ya shamba, anaye ishi pale, wakati nyumba ilijengwa na pia pesa gani za kiserikali- taxes - ambazo zimelipwa. Pia unaweza kujua kama mwenyewe anataka kuiuza shamba hilo. Utapata habari yote pale. Nani anayetengeneza habari hiyo yote? Ni Wakenya. Lakini ukisema kuwa kama Wakenya tuketi na tujaribu kupata suluhisho kuhusu maswala haya yote, haiwezekani. Kwa sasa, unapata shamba moja lina hati miliki za ardhi 12. Unapata mama mjane ambaye anafukuzwa katika shamba lake. Unapata Chifu pia hawezi kumsaidia. Hili jambo la kusuluhisha shida za shamba nchini lazima liangaziwe. Kamati husika inafaa kujaribu iwezekanavyo ili tuketi Pamoja. Wengi wetu ni wazee na tunafahamu mambo haya. Tutafute suluhisho ili Wakenya wajue kuwa sheria inalinda mali na rasilimali yao. Asante."
}