GET /api/v0.1/hansard/entries/1372471/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1372471,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372471/?format=api",
"text_counter": 43,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Shida ya ukosaji wa hati miliki katika eneo la South Ngariama linashughulikiwa na Waziri. Ila shamba likikaa kwa muda bila hati miliki ina madhara yake. Tutashikana kama viongozi na kuhakikisha kwamba waliokuwa kwenye shamba lile wanaangaliwa. Nitalinganisha jambo hili la Muthanthara na tukio la mpaka uliokuwa unawekwa kati ya Tharaka-Nithi na Embu. Watu kwenye mpaka ule ni Waembu, mipaka ikiwekwa walivukishwa wakawa upande wa Tharaka-Nithi. Bado wanajihusisha na Waembu na wanavuka mpaka kupiga kura ila mashamba yako kwenye Kaunti ya Tharaka-Nithi. Hili jambo limekawia kwa muda mrefu bila kusuluhishwa. Wakati mwingine linaleta maafa. Mmeona maafa Kirinyaga. Si lazima mtu apewe shamba kulingana na kule wametoka. Wale ambao wamemiliki lile shamba kwa muda mrefu, wapewe hati miliki ili kuhakikisha kuna usawa kwa Wakenya wote."
}