GET /api/v0.1/hansard/entries/1372933/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1372933,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372933/?format=api",
"text_counter": 155,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi County, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Gertrude Mwanyanje",
"speaker": null,
"content": "ama full scholarship, nafanya kule Kilifi. Kufikia saa hii, sijapata pesa zangu za mradi wa NGAAF yaani robo ya kwanza na robo ya pili, wala pesa za bursary . Niliwaahidi watoto walioko ofisini mwangu kuwa nitawalipia bursary na kuwapa full scholarship kufikia wiki jana kabla Bunge halijafunguliwa. Pesa hazijaingia katika account yangu. Wawakilishi wa Wanawake hapa hawana pesa. Ni nini Serikali yetu yatakia kizazi chetu cha watoto wanaoenda shule? Twasema elimu kwanza. Pale Kilifi, najulikana kama ‘Mama lao’, ‘Mama G’, na ‘Elimu Kwanza ndani ya Kilifi’. Sijaweza kutimiza ndoto yangu ya kuwalipia hawa watoto karo ya shule. Ninaonekana mwongo. Tulizungumza kuhusu sodo Waziri Machogu akiwa hapa. Mpaka leo, hatujaona shilingi milioni 470, ambazo ni shilingi milioni 10 kwa kila jimbo. Umeelezewa mambo ya hedhi na wasichana. Wengine wanapata mara tatu, mara nne ama tano kwa wale wanaokula vizuri kwao. Siyo aibu. Nataka kumwambia Mheshimiwa aliyesema ni aibu kuwa hakuna aibu ya hedhi iwe ni kwa baba ama mama. Walio hapa ni wazazi wa watoto wa kike. Aibu ya hedhi inatokea wapi? Wao ni mabwana walio na mabibi wanaopata hedhi. Aibu ya kuzungumzia mambo ya hedhi ndani ya Bunge yatoka wapi? Mhe Spika, tunataka pesa hizi ziweze kutolewa na watoto wetu waweze kuenda shule ili tutimize ndoto yetu ya mpito wa asilimia 100. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}