GET /api/v0.1/hansard/entries/1373115/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1373115,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373115/?format=api",
"text_counter": 337,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda. Na mimi kama Mama Kaunti wa Mombasa, naomba kutoa mchango wangu. Inasikitisha sana hata baada ya taifa hili kupata Uhuru, akina mama wa taifa hili bado hawana uhuru. Akina mama wanauliwa usiku na mchana. Sote tunajua mama ni pambo la ndoa, mama ni pambo la mwanaume, na mama ni pambo la ndani ya nyumba. Mama ni mlezi. Sisi akina mama ndio tunaoshika mimba, tunakula udongo, tunakula matope, tunatapika, tunapitia ile hali yote duni ili tuweze kuzaa mtoto ambaye pengine ni mtoto wa kiume. Inasikitisha kuwa leo mama anadhalalishwa katika taifa hili. La kusikitisha zaidi ni kuwa hata yule ambaye ni Waziri wa Usalama hajajitokeza kuzungumzia mambo haya ambayo yanatendeka. Na mimi napenda tuweze hata kumuita ndani ya Bunge hili ili aweze kutuambia visa hivi ambavyo vimetokea ambapo watoto wetu wa kike wameuliwa. Tumesikia kuhusu Sharon. Imetugusa sisi sote. Juzi Mombasa kuna mwanamke mama mtu mzima amechinjwa kama vile anavyochinjwa ng’ombe na mjukuu wake wa kiume. Lakini mambo hayo yanapelekwa chini ya maji. Mambo haya hayazungumziwi Mhe. Spika wa Muda. Mimi ningependa Waziri wa Usalama aje hapa atuambie anafanya kitu gani kuhakikisha kuwa visa hivi vinaweza kuchukuliwa hatua ili mambo haya yaishe. Kuna mambo mengi ambayo yanatendeka ndani ya social media kwenye mitandao. Sisi akina mama tunatukanwa na watu tunaowajua. Atakupa matusi mpaka yale ya mvunguni. Roho zetu ni ndogo. Roho zetu ni dhaifu. Kuna watu wengi wametoka kwenye mtandao, wameenda wakafunga kamba wakajiua kwa sababu yale mambo ambayo wanaambiwa kwenye socialmedia ni mambo ya kudhuru, kuvunja moyo na kutoa hadhi yao. Ni mambo ambayo yanasumbua mtu hata usingizi hawezi kupata. Na ndio mambo ambayo sisi katika Bunge hili inafaa tuangalie. Hata kama kuna freedom ya speech, haya mambo yamefika mbali. Na leo watoto wetu wanaitwa kwenye mitandao. Hao ambao umewaona wameuawa ni watoto ambao wametongozwa kwenye mtandao. Mtu anampigia simu ama anamchat na akisha mchat anamwambia njoo mahali fulani. Kisha anachukua advantage kuwa yule amekuja na anamuua kiukatili na anatoa sehemu za mwili na anaondoka nazo. Na la kutamausha ni kwamba Serikali imenyamaza. Mimi kama Mama Kaunti wa Mombasa nahisi uchungu sana. Ni wakati sasa Serikali ianze kuchukua hatua. Ni wakati ambapo Serikali ianze kusikia sauti za akina mama. Tena mimi ningependa kuwapongeza sana wale wabunge wanaume ambao wako kwenye Bunge hili wakati huu ambapo tunatoa mchango wa huu mjadala. Namshukuru ndugu yangu Junet. Nimemwona Kiarie pale na Wabunge wanaume. Nyinyi mmesimama na akina mama na mimi leo nawapongeza. Nawapongeza sana. Bunge limebaki tupu. Watakuja na mijadala yao na watataka sisi akina mama tuwatetee ilhali tunauliwa. Tutasimama na wale viongozi ambao wanasimama na akina mama. Ni wakati ambao lazima tuzungumze kwa sauti moja. Mwanamke anafaa aheshimiwe. Mtoto wa kike anafaa adhaminike. Haya mauaji tunasema yaweze kusitishwa. Tumezungumza tukilalamika siku zote. Nenda kwenye mahakama zetu, kesi zimejaa. Mtoto mdogo amelawitiwa. Mtoto ameuawa. Lakini hata wale majaji wa kutosha pia hatuna. Na mimi kama Mama Kaunti namlilia Jaji Mkuu wetu. Kule Mombasa tuongezee majaji. Hizo kesi ziko. Unapata babu amelawiti mjukuu wake na ametoka yuko kule anauza barafu. Mtoto anakaa na aibu. Mtoto wa darasa la sita . Yule mzee ako nje tu, anacheza ile kera, anafanya mambo yake, yake yakimwendea. Yule wa Sharon tunaona tu huku nje. Ako tu. Hatujapata mtu hata sasa ambaye alimuua wala kesi haijaamuliwa kwa vyovyote vile. Yule mama alikufa na mtoto wake. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}