GET /api/v0.1/hansard/entries/1373139/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1373139,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373139/?format=api",
    "text_counter": 361,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii niunge mkono Hoja ilioko mbele ya Bunge hili kuhusu mauaji ya wanawake ambayo yametanda katika taifa hili letu la Kenya. Pia, nampongeza dadangu, Mhe. Passaris, Mbunge wa Kaunti ya Nairobi. Pia nalipongeza shirika la Kenya WomenParliamentary Association (KEWOPA), ambalo tangu juzi limekuwa likitilia pondo swala hili. Wiki hii, Wabunge wanawake wa Bunge hili tunavalia mavazi ya rangi nyeusi. Hii ni ishara tosha ya kuwa wanawake wako katika msiba mkuu ambao umelisibu taifa hili juu ya mauaji ya wanawake wanaouliwa kiholela. Mambo ambayo wanawake wanayoyapitia yamekuwa kama mchezo wa paka na panya. Natoa rambirambi zangu kwa uchungu mkubwa sana nikiwa mwanamke ambaye anajua uchungu wa uzazi. Poleni sana kwa familia ambazo zimefikwa na misiba. Kuona mtoto wako wa kike ameuawa kiholela, pengine mtoto uliyemsomesha vizuri, anafanya kazi yake nzuri, na anaishi maisha yake mazuri; na wewe kama mzazi unafurahi ukiona mtoto wako wa kike anaendelea vizuri. Hakuna uchungu kama wa kumpoteza mtoto, uchungu ambao The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}