GET /api/v0.1/hansard/entries/1373140/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1373140,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373140/?format=api",
"text_counter": 362,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
"speaker": null,
"content": "wanawake huwa wanapitia. Sijui vile wanaume huwa wanasikia. Ni uchungu mkubwa kumpoteza mtoto wako kwa mauaji ya kikatili. Unaona msichana ameuawa, amekatwakatwa kama nyama ya mshakiki na imewekwa kwa mfuko wa karatasi. Hujui huyo muuaji alikuwa ana unyama kiasi gani. Sisi Waislamu tunasema dunia imefika mwisho. Haya ni mambo ambayo yametabiriwa katika Qur’ani tukufu. Utafika wakati binadamu watageuka kuwa wanyama na wanyama watageuka kuwa binadamu. Ni uchungu ulioje kwa Wakenya na wanawake kwa ujumla, na pia nimeona wanaume wakituunga mkono kwa sababu pia wao wanazaa watoto wa kike. Usalama wa watoto wetu uko wapi? Naiomba Serikali yetu ilioko--- Najua hii Serikali ingekua ya Mhe. Raila Amolo Odinga, haya mambo yangekuwa rahisi. Yule mzee ana huruma nyingine tofauti ya uzazi. Nashangaa nikiona Serikali haijafungua mdomo tangu majuzi haya maneno yalipoanza kutendeka. Kweli hawa ni wazazi? Kweli wanazaaa watoto wa kike? Kweli hawa wanazaa watoto hata wa kiume? Kwa sababu dhuluma ni dhuluma, Mhe. Spika. Siyo dhuluma ya mtoto wa kike pekee iliyo chungu. Dhuluma ya kumpoteza mtoto ni dhuluma, na ni uchungu kwa mzazi yeyote ambaye amezaa. Waswahili wanasema mwerevu---"
}