GET /api/v0.1/hansard/entries/1373156/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1373156,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373156/?format=api",
    "text_counter": 378,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uzima, nguvu na uhai kuweza kurudi tena katika Bunge hili baada ya likizo ndefu. Nami pia nasimama kulaani kitendo cha mauaji ya wanawake. Hili si swala la viongozi wa kike pekee, bali ni wajibu wa Taifa nzima kulaani hawa mashetani wachache ambao wamechipuka sasa na wanaua wanawake kwa kuwakatakata. Sio wanaume wote wabaya; wengi wao ni wazuri. Mimi nimeishi na mke wangu zaidi ya miaka 30, na bado tunapendana sana kama watu waliooana jana. Pia nina binti mmoja, na tunaishi vizuri sana. Kwa hivyo, hiki ni kitendo cha mashetani. Hata mila zetu haziruhusu kutoa uhai wa mwanamke au binadamu yeyote yule. Katika dini ya Kiislamu, kama kuna vita vikali, tumekatazwa kuua wanawake na watoto. Kwa hivyo, wanaoua wanawake ni mashetani. Ni ombi langu kwa Kurugenzi ya Ujasusi na Jinai, na polisi wa kawaida kushirikiana ili wazuie maafa haya. Na kama jambo kama hili litakuwa limefanyika, isichukue zaidi ya wiki kuwashika wahusika. Hivi ndivyo tutakavyozuia maafa haya. Ikiwa tutawaacha wahusika kukaa miezi miwili kama hawajashikwa, tunawapa mashetani hao wengine nafasi za kuendeleza maafa haya. Kwa sababu wenzangu wengi bado wanahitaji kuzungumza, nasimama kulaani kitendo hiki. Naomba Mungu awalaze mahali pema waliotangulia. Ahsante sana."
}