GET /api/v0.1/hansard/entries/1373159/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1373159,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373159/?format=api",
    "text_counter": 381,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Mashariki inakumbwa na shida nyingi sana, lakini, alhamdulilahi, tunashukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa kwetu hatujashuhudia mauaji ya wanawake. Hivi leo tunalia na Wakenya wengine. Si sawa wanawake kuuawa. Pia si sawa sisi kulaumu tu Serikali. Kwa maoni yangu, tunazo sheria nyingi kuhusu jambo hili, lakini hazitumiki. Jambo ambalo nataka kutilia mkazo sana ni namba ile ya dharura ya 1195. Wakenya wengi hawajui kuwa kuna namba ya dharura inayoshughulikia maswala haya. Namba hii hutumika masaa 24, na pia inapigwa bila malipo. Unapopatikana na tatizo lolote kama la ubakaji, ukipiga namba hii, unapata nusra na watu wa kukusaidia hata kama ni kwa mawazo au uelekezi. Naomba viongozi wote walioko hapa Bungeni waitangaze namba hii kila tunapoenda mashinani. Tatizo hili sio la wanawake pekee. Naomba Serikali iipatie nguvu namba hii. Kama ningeruhusiwa, ningeipiga sasa hivi ili kutoa mfano. Ni muhimu iweze kujulikana kote kwa kuwa ni ya msaada mkubwa kwa wanawake wetu ili wasipate shida kufikia mpaka kuuawa. Pili, kuna mikakati ambayo imewekwa tunayostahili kuboresha. Katika kila kituo cha polisi, kuna desk ya Gender-Based Violence (GBV) . Kama Wabunge na Serikali kwa ujumla, tunafaa kuelimisha watu wetu kuhusu desks hizi, na pia kuziboresha. Na je ni vipi tutaziboresha? Nilipokuwa Mwakilishi wa Wanawake Bungeni, nilitembelea kituo kimoja cha polisi, na hii desk ya GBV ilikuwa bila mtu. Ni muhimu desks hizi ziwe active . Pia Serikali kupitia kwa Inspector-General inapaswa kuajiri polisi wa kike wengi watakaosimamia desks hizo. Sio eti mwanamke akipigwa na mwanaume, anahudumiwa na mwanaume katika kituo cha polisi. Wanaume wengine hutetea tu wanaume. Kwa hivyo, ni muhimu desks hizo ziwezeshwe zaidi na pia waajiri wanawake zaidi. Mhe. Spika wa Muda, napinga vikali mauaji ya wanawake nchini. Wakati huu, naona wanaume kutoka sehemu zingine, kama unakotoka Spika wa Muda, mje Lamu muulize wanaume wetu kwanini hawawapigi au kuwaua wanawake. Ni kwa sababu wanatupenda sisi wanawake, na wanajua kuwa mwanamke ni kitulizo cha roho na hakuna haja ya kumpiga. Ahsante."
}