GET /api/v0.1/hansard/entries/1373383/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1373383,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373383/?format=api",
    "text_counter": 205,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi North, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Owen Baya",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Mswada ambao upo katika Sakafu ya Bunge leo ni Mswada muhimu sana unaohusu wazee wa vijiji na wazee wa Nyumba Kumi. Ninamshukuru rafiki yangu, Mhe. Malulu Injendi kwa kuleta Mswada huu. Huu ni Mswada ambao mimi niliuleta katika Bunge la Kumi na Mbili lakini haukufanikiwa. Niliuleta tena katika hili Bunge la Kumi na Tatu lakini nikapata ndugu yangu amenitangulia mbele, nikasema tuungane tusukume Mswada wake. Wazee wa vijiji hapa Kenya wanapata shida sana. Wao huamka mapema asubuhi wakimbie kwa ofisi ya chifu ili wafanye kazi ya Serikali. Wao huamshwa usiku wafanye kazi ya Serikali. Kila mtu hutafuta wazee wa kijiji, hata wanasiasa. Wazee wa kijiji wanaporudi nyumbani jioni, wanarudi mikono mitupu. Watu wao hulala njaa ilhali wao hushinda kazini kwa sababu ile kazi wanafanya hawalipwi. Huu ni wakati mwafaka kama Bunge la Kumi na Tatu kuwanusuru wazee wa vijiji. Ninaamini kwamba Serikali iko na pesa. Pesa hizi zikitafutwa, wazee wa vijiji Kenya nzima watapata pesa kwa kulipwa mshahara kama vile wanavyolipwa Assistant Chief na machifu ili nao wakae vizuri maanake wanafanya kazi kubwa sana. Pale kwangu Kilifi North, kuna mzee amefanya kazi ya mzee wa kijiji kwa karibu miaka kumi. Mzee huyo anaitwa Chembakeke. Ametumikia wananchi kama mtu ambaye yuko kazini. Amewacha kila kitu ili afanyie Serikali kazi lakini watoto wake hawaendi shule kwa sababu hana pesa za kuwalipia karo. Huyu mzee hukosa pesa ya kununulia mkewe dawa anapogonjeka kwa sababu yuko kazini akifanya kazi ya Serikali. Pale Chifu na A ssistant Chief wanakoenda, wao hutaka kwenda na wazee wa vijiji na huwa wanaenda nyumbani bila malipo yoyote. Kwa hivyo, wakati mwafaka umefika wa kuangalia wazee wetu wa vijiji ili walipwe. Kila wakati tunapoenda mikutano kama Wabunge, wazee wa vijiji husema kuwa wametufanyia kazi lakini hawajui wataanza kulipwa lini. Kuna wale polisi wa Kenya Police Reserve (KPR) ambao hulipwa marupurupu. Ile kazi wanayofanya ni kama kazi ya wazee wa vijiji lakini wazee wa vijiji hawalipwi chochote. Tukiendelea kuwaacha wazee wa vijiji bila malipo, tutasambaza umaskini. Serikali yetu inafaa ipunguze umaskini, lakini inasambazaa umaskini kwa sababu inaruhusu watu wafanye kazi bila malipo. Wazee wamejitolea kweli kweli kwa sababu wanapenda community . Wanafanya kazi zao kwa kujitolea lakini mwisho wa siku wanaenda nyumbani bila chochote na familia zao zinabaki kwa umaskini. Serikali haiwasaidii hawa wananchi. Siku moja nilisema kuwa ni afadhali ikiwa hawa wazee wote wataacha hizi kazi. Wanaweza kutafuta mambo mengine ya kufanya ambayo yatawapa mapato. Siku saba za wiki, wazee wa vijiji huwa kazini wakiwahimiza watoto wa wazazi wengine waende shule, haswa wakati huu ambao tunaongea kuhusu 100 per cent transition . Ni wazee wa vijiji ambao huzunguka kila mahali wakiwaambia watoto waende shuleni ilhali watoto wao wanabaki nyumbani kwa kuwa hawana karo na Serikali haiwangalii. At least hata kama hakuna pesa, wazee wa vijiji wajue kuwa wana privilege fulani. Kwa mfano, hata kama watakosa pesa, wajue kuwa watoto wao watasoma bila kuulizwa karo. Watoto wao watasomeshwa kwa sababu wazee wa vijiji wanatumikia Serikali. At least tutasema kuwa hii ni kitu watakacho faidika nacho. Wazee wa vijiji wanapojitokeza kuwatafuta watoto ambao hawajaenda shule ili waende shule, wanapowapeleka watoto hao shuleni, headmasters huwa hawakumbuki kuwa hao ni wazee wa vijiji wawaambie watoto wao wasome shuleni bila kulipa karo. Hao huwaambia walipe karo. Kwa hivyo, hakuna faida yoyote hapa Kenya ya kuwa mzee wa kijiji. Huu Mswada ambao ndugu yangu, Mhe. Malulu Injendi – Mheshimiwa mzuri sana anayewafikiria na kuwajali Wakenya – ameleta, ni Mswada muhimu sana. Ninaomba Bunge hili lipitishe huu Mswada. Bajeti itakapoandaliwa mwaka huu, tuwaambie wanakamati wa Kamati ya Bajeti na Uidhinishaji wa Matumizi Pamoja na Mhe. Ndindi Nyoro kuwa ni lazima waweke bajeti ya wazee wa vijiji katika bajeti ya mwaka huu ili wazee wa vijiji wazidi kufanya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}