GET /api/v0.1/hansard/entries/1373384/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1373384,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373384/?format=api",
"text_counter": 206,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi North, UDA",
"speaker_title": "Hon. Owen Baya",
"speaker": null,
"content": "kazi na wapate pesa ya kukimu maisha yao na familia zao. Ninakumbuka nilipopendekeza Mswada huu, kuna mambo yaliyojitokeza. Usipolipa wazee wa vijiji pesa, utakuwa unasambaza corruption kwa sababu, wazee wa vijiji watakapokuwa wanakutana kwa mabaraza ya kuamua kesi, watakuwa wanaambiwa watapewa “kitu kidogo” ili waamue kesi kwa manufaa ya wachache. Kwa sababu hawalipwi, wazee wataanza kutafuta pesa kwa njia zingine ambazo hazifai. Ikiwa tutaendelea kuwa na wazee wa vijiji wanaofanya kazi bila kulipwa, tutakuwa tunaleta ufisadi katika hizo kazi. Kama wazee watafanya kazi na wasilipwe wanapoamua kesi katika mabaraza, atakao wapa “chai” ndiye atakayepata haki. Yule ambaye hatakuwa na chochote hatapata haki. Kwa hivyo, tuwafanyie haki wazee wa vijiji kwa kuwalipa. Tusipowalipa, watatafuta mbinu na njia za kupata pesa ambazo si halali. Tukitaka kumaliza corruption katika wazee wa vijiji, ni lazima walipwe. Ninataka kuwa katika mstari wa mbele kwa kusema kwamba, katika bajeti ambayo tutapitisha, wakati ambapo Budget Policy Statement (BPS) itakapokuja kuwe na line itakayosema kuwa ni wakati mwafaka wa kuwalipa wazee wa vijiji na hali hio iendelezwe mpaka itakapoingia kwa bajeti. Tunaiambia Kamati ya Administration and National Security inayoongozwa na Mhe. Tongoyo ikae kidete. Wakipewa fursa ya kutengeneza bajeti, waweke pesa ya wazee wa vijiji iwe Ksh 5billion, 8 billion au 10 billion per year . Kenya ilitumia Ksh10 billion kufanya maneno ya “reggae.” Ten billion ilitumika kwa Building Bridges Initiative (BBI) . Hiyo Ksh10 billion ipatiwe wazee wa vijiji. Tukiwapa bajeti, tuhakikishe kwamba kuna usalama na utulivu katika hii nchi na vijiji vyetu vinakuwa managed vizuri. Huo ndio mchango wangu katika maneno ya wazee wa vijiji. Kwa hivyo, ninafurahia kuwa tumeleta huu Mswada kwa Second Reading . Tuupitishe kabla bajeti haijamalizwa katika hili Bunge ili wazee wa vijiji waanze kupata matunda ya kazi yao. Ninaunga mkono mia fil mia Mswada huu ambao umeletwa na Mhe. Malulu Injendi, mtu mzuri. Asante."
}