GET /api/v0.1/hansard/entries/1373386/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1373386,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373386/?format=api",
"text_counter": 208,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kitui South, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr) Rachael Nyamai",
"speaker": {
"id": 13374,
"legal_name": "Richard Ken Chonga Kiti",
"slug": "richard-ken-chonga-kiti"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia swala hili muhimu ambalo limeletwa na Mhe. Malulu Injendi. Kabla sijachangia, ningependa kuchukua fursa hii kuwatakia wakatoliki wa constituency ya Kitui South, Wakenya na dunia nzima Jumatano ya majivu yenye baraka. Pia, ninawatakia wakati mzuri wa lent. Ninachukua fursa hii kuwashukuru wanawake wa Bunge leo kwa kuvaa nguo nyeusi kwa kuwakumbuka wasichana na wanawake wetu ambao waliuwawa katika hali tatanishi katika nchi yetu ya Kenya na sehemu zingine za dunia. Wazee wa vijiji ni jambo ambalo limezungumziwa sana katika Bunge hili lakini hatujachukua step kubwa ya kuwapa kiinua mgongo chao ama kuwalipa kwa kazi wanayoifanya. Hawa ni wazee na wengine wao ni wazee waliopitisha miaka sabini. Ninashukuru Serikali kwa sababu wengine wao wanapata pesa ya uzeeni kutoka kwa Serikali. Hata hivyo, wazee wa vijiji wanafaa kushughulikiwa wakati huu kwa sababu hao ndio hukutana na mambo mabaya ambayo hufanyika katika vijiji vyetu. Mhe. Naibu wa Spika, wamekuwa wakifanya kazi hii. Wengine wamefanya miaka kumi na kumi na mitano. Wengine wamefanya kazi hii tangu wawe watu wazima. Kwa hivyo, ningependa kushirikiana na wenzangu. Huu ni wakati wa Serikali ya Kenya Kwanza kuwezesha wazee wa vijiji wapatiwe pesa, ili tuwashukuru kwa ile kazi wanafanya kila siku wakiwa na machifu na manaibu wao. Tunajua kwamba machifu na manaibu wao wanapatiwa pesa kila mwezi na mafuta ya kwenda mahali kuna matukio. Hawa wazee wamejitolea kwa miaka mingi. Kwa hivyo, ningependa kushirikiana na Wabunge wale wamezungumza mbele yangu. Tuwapatie pesa ndio waone kazi ambayo wamekuwa wakifanya ni muhimu. Saa hii tunazungumzia kuhusu social health insurance. Wazee hawa watasaidiana na Serikali ili watuambie ni nani anaweza lipa hii mia tatu ambayo italipwa na ni nani hawezi katika jamii. Kwa hivyo, hawa wazee wa vijiji ni muhimu sana The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}