GET /api/v0.1/hansard/entries/1373387/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1373387,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373387/?format=api",
    "text_counter": 209,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kitui South, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr) Rachael Nyamai",
    "speaker": {
        "id": 13374,
        "legal_name": "Richard Ken Chonga Kiti",
        "slug": "richard-ken-chonga-kiti"
    },
    "content": "katika kusukuma mbele mambo ya social health insurance. Pia, hawa wazee wanatumiwa sana kueneza mambo ya Serikali zote katika nchi ya Kenya. Katika Serikali hii, wataeleza watu umuhimu wa ujenzi wa nyumba na sera zote. Ninaunga mkono wapatiwe kiinua mgongo na tuwashukuru kwa kazi nzuri ambayo wanafanya. Hata tukizungumzia mambo ya ushauri, hawa wazee ndio wanafika kwanza mahali mtu amekufa ama ameuawa. Wasichana wengi wanauawa katika hoteli wakati huu. Pia, wanafika wakati watu wamepigana na kuumia. Hatufikiri shida wanapitia akilini. Hata kama hakuna kitu kingine tutawafanyia, wacha tuwapatie pesa ndio waone kazi wanafanya ni muhimu nchini. Wengi wamengojea sana. Wale wana miaka themanini wamengojea kwa miaka ishirini. Wale wana miaka sabini, wamengoja tangu wawe na miaka hamsini. Ninaomba Kamati ya Bajeti ambayo inasimamiwa na Mhe. Ndindi Nyoro na Kamati ya Idara ya Utawala na Usalama wa Taifa ambayo inasimamiwa na Mhe. Tongoyo washikane. Pia, sisi sote tuseme wazee wa vijiji ni muhimu sana katika Kenya yetu. Wanaangalia mambo ya nyumba kumi na wasichana ambao wamepata mimba na hawajaenda shule. Pia, wanapeana ripoti ya wazazi ambao wamekataa kupeleka watoto wao shuleni, ili asilimia mia moja ya watoto kutoka shule za msingi wajiunge na shule za upili. Mhe. Naibu wa Spika, ninashukuru kwa kunipatia nafasi hii. Ninaunga mkono kabisa kwamba wazee wa vijiji watambuliwe kwa maneno na wapatiwe kiinua mgongo. Asante."
}