GET /api/v0.1/hansard/entries/1373389/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1373389,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373389/?format=api",
    "text_counter": 211,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Migori County, Independent",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Mhe. Naibu wa Spika, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ili nipeane maoni yangu. Ninawaambia wenzangu wote happy new year. Tunashukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kurudi salama sisi sote na afya nzuri. Hawa wazee wanachangia katika jamii. Wanajua watu wa vijiji kuliko hata polisi na wakuu zaidi ambao wanalipwa. Wao niwamaana sana kwetu. Tukitaka kushika mwizi, wanajua kabisa mwizi ni nani. Saa zingine, mahakama inapata nafasi, lakini inakosea kumtambua yule mbaya. Mzee wa Kijiji anajua familia kuanzia utotoni. Anaweza shuhudia na aseme Fatuma amekuwa mtu fulani tangu azaliwe na ukweli upatikane. Wanachukua fursa nyingi sana. Ni kama watu ambao wanafanyia Mungu kazi kwa sababu hawalipwi chochote. Wanaishi maisha mabaya. Ni maskini hata kuliko wanaowafanyia kazi. Tunahimiza Serikali ya Kenya ichukue nafasi kubwa sana kuwatetea hao wazee, ili wazidi kutusaidia. Wakati mambo ya ugaidi yalizidi sana, wazee walitusaidia sana kutambua vijana wabaya na wazuri. Pia, wanatusaidia kuhimiza utamaduni wetu. Kila siku wanafunza wadogo wetu. Wanatuambia utamaduni wetu ulianzia wapi na unaelekea wapi. Kwa hivyo, hawa wazee wanafaa kuchungwa. Zaidi ya haya, kwa sababu ya umri wao, wana afya ambayo sio nzuri, lakini hawawezi kupata matibabu hata katika hospitali za Serikali. Ninaomba matibabu ya wazee ipewe kipaumbele ili watibiwe hospitali bila malipo yeyote. Hawana bima na Serikali haitaweza kuwalipia. Ikiwezekana, walipiwe bima ama wapewe fursa ya kuingia hospitali yeyote kutibiwa pamoja na familia. Tukiongea kuhusu wazee, tusifikirie ni wa kiume peke yake. Kuna wa kike pia. Watambulike na wapatiwe nafasi ya kupata malipo madogo ya kujimudu kwa kuwa ile kazi wanafanya kwa jamii hawawezi kulipwa mshahara wa kutosha. Ni kuwashukuru tu kwa kazi wanayotusaidia katika jamii. Kama Serikali na Bunge la Kitaifa, tujaribu tupitishe Mswada ambao utawezesha hawa wazee wapate nafasi nzuri ya kutusaidia na motisha ya kufanya hii kazi. Tusipowapatia kitu kidogo cha kujimudu, tunaeneza ufisadi, kwa sababu itabidi waombe watu kuku ndio wafanye ile kazi wanafaa kufanya. Wanapotaka kusafiri, hawana nauli. Inabidi waombe. Hiyo inakaa ni kama mzee anakuomba hongo. Hawa ni wazee ambao wanahekima, heshima na hawataki waonekane ni kama wanaomba. Serikali ijaribu sana tuwatetea hawa wazee. Itakuwa baraka kwetu kama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}