GET /api/v0.1/hansard/entries/1373443/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1373443,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373443/?format=api",
"text_counter": 265,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mandera South, UDM",
"speaker_title": "Hon. Abdul Haro",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii nichangie Mswada huu muhimu kuhusu uratibu wa Serikali kuu wa marekebisho ya sheria ili kuhakikisha kwamba wazee wa mitaa wameweza kuzingatiwa katika sheria. Ningependa kuchukua fursa hii kumshukuru Mhe. Malulu Injendi kwa kuweza kuuleta Mswada huu wakati huu ambapo ni muhimu zaidi katika nchi yetu ya Kenya. Wazee wa mitaa ni nguzo muhimu sana katika jamii yetu. Wamekuwa wakichangia katika sekta zote za jamii zetu humu nchini. Hata wakati tuko na janga kama lile lililotekea kule Embakasi siku chache zilizopita, ama mafuriko kama yale yaliyokuweko wakati wa El Nino, wazee wa mtaa wamekuwa msitari wa mbele wa ulinzi ili kuhakikisha kwamba usaidizi ama msaada ambao umetolewa na Serikali ama mashirika yasiyo ya Serikali umeweza kuwafikia wale ambao wanahitaji msaada ule. Wale wazee ndio huwa wanatumika kuwatambua wale ambao wameathirika zaidi. Vile vile, ndio wanaotumiwa kuwatambua wale ambao wanafaa kusaidiwa wakati janga kama hilo linapotokea. Katika hali ya usalama, haswa sisi tunaotoka sehemu ambazo ni za watu wanaohama na mifugo wao, tumekuwa na changamoto nyingi za kiusalama, kama vile ukosefu wa sehemu za malisho na maji ya mifugo wetu. Wakati mzozo unapotokea, wazee wa mtaa wamekuwa katika safu ya mbele kuhakikisha kwamba tumepata utangamano na tuko na amani na usalama katika sehemu zetu za malisho na jamii zetu zinaendelea kuishi kwa amani. Kwa hivyo, ni muhimu kuwatambua wazee hawa maanake siku nenda siku rudi wamekuwa wakifanya kazi ya kusaidia Serikali, jamii na mashirika yasiyokuwa ya Serikali. Kazi yao huwa ya kujitolea. Hakuna wakati wowote ambapo wanapewa mshahara ama kiinua mgongo. Hata ukiangalia katika idara zetu za mahakama, ninafikiri wazee hawa wamechangia sana katika kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwa Wakenya wote. Wamekuwa wakishirikiana kusuluhisha kesi nyingi ndogo ndogo ambazo zingeishia kufika mahakamani na zijaze korti na kuchelewesha kesi nyingine nyingi. Watu wengi wangekaa miaka mingi bila kupata haki yao katika idara za mahakama kwa sababu ya hizo kesi kuchelewa zikiwa nyingi. Hawa wazee wanachangia kuhakikisha kwamba asilimia 50 ya kesi ambazo zingeenda mahakamani zimesuluhishwa mitaani. Mchango wao ni mkubwa na ni lazima tuhakikishe kwamba wanafidiwa. Ninamshukuru Mhe. Malulu Injendi kwa kuuleta Mswada huu ili kuhakikisha kwamba yale ambayo tutakubaliana kuwalipa hawa wazee inawekwa katika sheria ili itumike kwa vizazi vya leo na vya kesho. Kuhusu gharama ya huduma ya wazee kama hawa, ninafikiri katika nchi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}