GET /api/v0.1/hansard/entries/1373444/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1373444,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373444/?format=api",
    "text_counter": 266,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mandera South, UDM",
    "speaker_title": "Hon. Abdul Haro",
    "speaker": null,
    "content": "hii tuna pesa nyingi. Tunaweza kutumia kiasi kidogo tu kuwalipa wazee hawa. Kwa mfano, tuko na kata ndogo 9,045 katika nchi hii. Hiyo kata ndogo kila moja ina mtu anaitwa naibu wa chifu. Tukisema wazee watatu wa mtaa waweze kusaidiana na naibu wa chifu na walipwe shillingi 5,000 kila mmoja, kwa mwezi, ni shillingi 135,000,000. Kwa mwaka, ni Ksh1.6 bilioni. Tuliwahi kuambiwa na Rais Mustaafu Uhuru Kenyatta wakati wa enzi zake; kwamba, Serikali ilikuwa ikipoteza Ksh2 bilioni kupitia ufisadi kila siku. Kuwalipa wazee wa mtaa Ksh1.6 bilioni kwa mwaka litakuwa jambo nzuri sana kwa nchi hii. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}