GET /api/v0.1/hansard/entries/1373448/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1373448,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373448/?format=api",
    "text_counter": 270,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Igembe South, UDA",
    "speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia Mswada huu. Pia, ninampa kongole Mhe. Injendi kwa kuona kuwa wazee hao wanafaa kushughulikiwa. Ninasimama kuunga mkono Mswada huu. Wazee hao wanachangia pakubwa katika vijiji vyetu kuhakikisha kuwa kuna usalama wa kutosha. Pia, wakati Serikali inafanya kazi kule mashinani, wazee hao wa Nyumba Kumi ndio wahusika wakuu. Kwa sababu wanafanya kazi kubwa na iliyo ngumu, ni vizuri sisi kama Wabunge tunaotengeneza sheria tuwasaidie ili waweze kupata hela baada ya kila mwezi ambazo zitakidhi mahitaji ya familia zao. Utagundua kuwa watoto wa wengi wa hao wazee wa Nyumba Kumi huwa na shida kubwa ya kupata elimu bora ilhali tunawatumia wazee hao kule vijijini ili kuhakikisha kuwa kila mtoto amejiunga na shule. Tunawatumia wazee hao kule vijijini kuhakikisha kuwa kuna amani na kuwatambua wahalifu wanaotekeleza uhalifu. Huwa wanahatarisha maisha yao wakati mwingine kwa sababu wanawafahamu wauzaji wa mihadarati au madawa za kulevya. Wanapopeana ujumbe kuhusu wahusika wakuu wa uraibu wa mihadarati au wanapoibua ile ripoti ama habari, huwa wanajiweka kwenye shida. Ni vyema sana wazee hao waangaziwe na Serikali ili waweze kupata angalau kitu ambacho kitaweza kusaidia familia zao kila mwezi. Jambo hilo litahakikisha kuwa wanafanya kazi hiyo kwa furaha ili vijiji vyetu viimarike zaidi. Watakapokuwa wanapata zile hela, watapata motisha zaidi ya kufanya kazi. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Mswada huu na ninawatakia wakaazi wa Igembe Kusini siku njema ya kusherehekea wapendanao."
}