GET /api/v0.1/hansard/entries/1373463/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1373463,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373463/?format=api",
    "text_counter": 285,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Rabai, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Kenga Mupe",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii nichagie Mswada huu. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu ambao umeletwa na Mhe. Malulu. Mswada huu wa kubuni halmashauri ya vijiji chini ya wazee wa mitaa na wazee wa Nyumba Kumi ni hatua ya kijasiri ambayo ni ya kudhamini na kutambua kazi nzuri ambayo wazee wetu wa mitaa na wazee wa vijiji wamekuwa wakifanya katika utawala na uratibu wa kitaifa. Wazee hawa wamekuwa wakifanya kazi nzuri kule vijijini. Ni wakati mwafaka hawa wazee wa mtaa na wazee wa vijiji ama wazee wa Nyumba Kumi waanze kulipwa kwa sababu hata DCC, ACC, C hiefs na A ssistant Chiefs wanawategemea sana kwa kuwapea ripoti ya mambo ya usalama. Ninachukua fursa hii ya kipekee niwapongeze wazee wa mitaa na wazee wa Nyumba Kumi kutoka eneo Bunge pamoja na machifu na manaibu wa chifu. Wamekuwa wakifanya kazi nzuri ya ushirikianao na ndio maana usalama umetiliwa maanani sana. Kutoka jadi wazee hawa wa mitaa na wazee wa vijiji wamekuwa wakifanya kazi. Tunajua wako na familia, wako na watoto ambao wanataka kwenda shule na pia wako na majukumu mengine. Lakini hawakuwa wanalipwa kwa kazi ile yote nzuri wamekuwa wakifanya. Umefika wakati Serikali kupitia Kamati Bajeti ya Bunge hili itenge pesa ambazo wazee wetu wa mitaa na wazee wa vijiji watalipwa maana ni Wakenya kama wale wengine. Shughuli zile zote ambazo zinafanywa na wazee wa mitaa na wale wa vijiji ni kama mambo ya elimu. Juzi wazee wote wa mitaa na wa vijiji walikuwa wanaenda nyumba kwa nyumba kuhakikisha kwamba hakuna mtoto hata mmoja amewachwa nyuma ili kuhakikisha watoto wote wameenda shule. Ninaunga mkono wazee wetu wa vijiji na wale wa mitaa walipwe mshahara kama Wakenya wengine. Asante."
}