GET /api/v0.1/hansard/entries/1373468/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1373468,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373468/?format=api",
    "text_counter": 290,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
    "speaker": null,
    "content": " Nimshukuru Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii nami pia niwe katika kumbukumbu za Bunge hili katika Hoja hii iliyoletwa na Mhe. Malulu. Inahusu vile wazee wa vijiji wanatumika vibaya na Serikali yetu. Bi. Spika wa Muda wazee wa vijiji ni watu muhimu sana. Tangu nizaliwe, nimeona wazee wa vijiji wakitufanyia kazi bila kuchoka. Wanafanya kazi hii ya kujitolea. Mpaka wakati huu nimekuwa mtu mzima na kiongozi, sijawahi kusikia mzee wa kijiji akipata ruzuku ya angalau kitu kidogo ili apate sukari ya siku. Ningependa kuiambia Serikali hii kwamba tuwajali wazee na akina mama wa vijiji. Hatutaki kusema ni akina baba peke yake wanaoongoza vijiji. Wazee wa vijiji ni wa kike na kiume. Katika sehemu ninayotoka, nimeona wazee wa vijiji wakifanya kazi ya kujitolea mpaka wengine wanapoteza maisha yao. Miaka mitatu iliyopita, Eneo Bunge la Msambweni, wazee wanne waliuawa siku moja. Watu wasiojulikana waliingia nyumbani kwao na kuwaua kwa kudhania kuwa wazee hawa ndio waliokuwa wakipeana habari kwa Serikali. Hadi sasa, familia za wazee hawa hazijalipwa fidia. Hii ni kazi ambayo ni ya kuvunja moyo. Wazee hawa hujitolea na kushughulikia shida zote za kiusalama vijijini. Mara nyingi, Serikali hutumia wazee hawa kuandikisha “ statements” kueleza yale yanayojiri katika vijiji vyao. Hii ni kazi ya punda kwa kuwa haina mshahara wala shukrani. Ninaomba Serikali hii iwatambue wazee hawa kwa kuwa wanafanya kazi nzuri bila mshahara. Wazee wengi wa vijiji wanaishi maisha duni. Wanaishi katika nyumba za makuti na nyasi ilhali hao ndio wa kwanza kuulizwa maswala yote ya usalama. Wao ndio hujua ni wageni wapi wamezuru vijiji vyao. Wanajua ni mama yupi amejifungua na kupata matatizo na alipelekwa hosipitali gani. Pia wanajua watu wanaogombana katika ndoa. Anaweza kukuambia kuwa mume na mke fulani walipigana jana na akaita polisi au kuwaita pamoja na kushuluhisha yeye mwenyewe. Mimi kama kiongozi wa kike ninaona ni udhalilishaji wa hali ya juu wa viongozi wetu walio nyanjani. Ninaomba Bunge hili, Kamati ya Bunge ya Fedha na Serikali kuu kusimama na wazee hawa na kuwapatia riziki. Tuwaone kama binadumu. Wengi wao ndio wametuwezesha wengine wetu kupata nafasi za kitaifa kama ubunge. Wabunge wengi hapa ukiwauliza, wasingefika hapa kama si kusaidiwa na wazee wa vijiji. Pia, wazee hawa waliunga mkono Serikali hii ya sasa wakijua kuwa labda mambo yatabadilika. Hoja hii iliangaziwa tangu 1963 tulipopata Uhuru na bado tunazungumzia hata sasa. Ni jambo la aibu sana. Ingekuwa ni mataifa mengine ya nje, swala hili lingekuwa limeshughulikiwa zamani na wazee wa vijiji kupata riziki na kuishi maisha ya heshima."
}