GET /api/v0.1/hansard/entries/1373683/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1373683,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373683/?format=api",
"text_counter": 190,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Mambo ya ujenzi wa nyumba ninafikiri yalianza kule mwanzo wakati wa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta. Aliweza kujenga nyumba upande mwingine wa Kibera, na ningependa kumpongeza kwa sababu watu walioingia kwenye nyumba zile ni wale waliokuwa wametoka kwenye nyumba zilizobomolewa. Wanalipa Ksh2,500 ama Ksh3,000 kila mwezi, mpaka watakapo kamilisha malipo yao ili wachukue zile nyumba. Mhe. Spika wa Muda, kwa sasa mambo yanayoendelea ni hujuma. Nyumba zabomolewa. Kwa mfano, juzi walibomolea watu wa Changamwe. Pengine nyumba zingine zitakuwa zao. Lakini hata kupatia wananchi notice imekuwa vigumu. Ningependa Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi, ambaye ameleta Mswada huu, atuelezee mama mboga na mwana"
}