GET /api/v0.1/hansard/entries/1373686/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1373686,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373686/?format=api",
    "text_counter": 193,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Ni dhahiri kuwa wafanyikazi wengi wa Serikali walikuwa wamechukua mikopo na kununua nyumba ambazo tayari wako nazo. Ni dhuluma kubwa sana kukatwa pesa za HousingLevy na yale mapeni hawawezi kuyatumia. Serikali iko na ardhi kubwa. Hata wananchi wengine maskini wana mashamba yao. Kama Serikali kweli inataka kujengea mwananchi nyumba, mbona wale ambao wanakaa kwenye nyumba za matope katika mashamba yao wasiende kuwajengea nyumba za kisasa kisha wawambie kwamba watakuwa wakilipa Ksh2,000 mpaka wamalize deni, ndio waweze kuishi ndani ya nyumba ambazo ni dhabiti? Yale tunayoshuhudia ni uvunjaji wa nyumba, kunyang’anya watu mashamba yao na kudhalilisha Wakenya ambao wanalia huko nje. Ninataka niulize swali moja tu. Kufikia sasa, Kenya inadaiwa Ksh12 trilioni. Juzi tumemskia Mhe. Rais akisema kwamba madeni yamekuwa mengi na kulipa imekuwa mtihani. Wewe unadeni linalokusumbua. Kwa nini wachukue pesa tena waende kuwekeza kwenye vitu ambavyo Wakenya hawana haja navyo? Wakenya wakipiga kura walitoka katika nyumba zao, hawakutoka msituni. Inafaa haya mapeni ambayo anachukua kujenga nyumba ayatumie kulipa madeni ndio tumuelewe. Madeni yanazidi kukua na wananchi wanalia pesa zao zinakatwa. Kwanza, ile Fuel Levy ya 16 per cent inatosha kufanya haya mambo yote. Kwa sasa, ameenda extreme . Tusizungushane huku na kule, Wakenya wamechoshwa na kirba goji goji kirba. Wanamtaka Mhe. Rais aweze kuongeza"
}