GET /api/v0.1/hansard/entries/1373693/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1373693,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373693/?format=api",
"text_counter": 200,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni, ikiwa mwalimu alikuwa anafunza darasani na hukumwelewa, sio shauri yangu. Mzazi aliyekulipia karo atakuuliza ukifika nyumbani. Huo wote ni ushuru unaotozwa wananchi. Kwa nini ushuru uongezwe? Tumia ule ushuru wa asilimia kumi na sita kufanya hayo mazagazaga yote ambayo unataka kufanya. Wakenya washadhulumika katika ile asilima kumi na sita wanayotozwa. Kwa nini tuwafinye tena na Housing Levy wakati hata bodaboda na mama mboga hawajui mambo ya mshahara? Maskini wa Mungu; nimeona wameingia hadi vibandani kutakuwaje nchini Kenya? Ukitaka taifa lako liende kwa udhabiti, punguza ushuru na uzidishe mazao. Ukizidisha mazao, Wakenya watakuwa na furaha ya kukatwa ushuru. Pengine wenzangu walioko upande wa Serikali wako na shida nyingi hadi imewabidi wafanye hivyo. Na kama vile maiti hukuwa na nzi, pia huifuata mpaka kaburini. Pengine mnataka msaidiwe pale juu lakini mjue kuwa mkirudi kule chini kwa wananchi, mtapigwa makatafunua na mtalilia shida zenu kule chini. Wakati umefika kwa Bunge hili kusimama na wananchi wa Kenya na liweke misingi thabiti ya kutetea mwananchi wa kawaida. Iwapo uko Upinzani au Serikalini, tafadhali simama na watu wako. Mwambie Rais kuwa hii Housing Levy imezidi. Atumie ile asilimia kumi na sita aliyoichukua aifanyie mambo yake lakini kwa haya mengine, amhurumie mwananchi wa kawaida. Ukiona kiongozi wa taifa anaenda kila mahali kisha anazomwa, sio ishara nzuri. Inamaanisha Wakenya wamechoka na wanahangaika. Sisemi kwa kuchukia ila kwa kutengeza. Kesho, Mhe. Rais atakapo kwenda kukaa kando pekee, atakubaliana nami kuwa mimi nilisema ukweli na atajua kuwa wenzake ndio wanaomdanganya na kuzidi kumdidimiza. Ninaongea kama mama aliyeuza sambusa na kufanya kazi kama house keeper kule Saudi Arabia. Sisi hatujui mambo ya mshahara kukatwa Housing Levy wala hatujui kunaendaje. Wasitumie majina ya mama mboga na mvuta mkokoteni kudhulumu wafanyikazi ambao mishahara yao inasoma “zero salary” wakati mwingine. Mhe. Spika wa Muda, Wabunge wenzangu na wananchi, mwambieni Rais ukweli. Mambo yanaenda yombo. Mambo kangaja huenda yakaja. Kenya inadidimia. Waheshimiwa wenzangu, msiingize Rais mahali pabaya. Hatuoni mama mboga au mvuta mkokoteni. Kuna Daktari, Mwalimu au Mkenya wa kawaida mahali ambaye anaskia amedhulumiwa na anaskia uchungu. Mambo ya Housing Levy yamekataliwa kortini. Kubali yaishe. Mulivyopewa uongozi, sisi tulikubali yakaisha. Hii Housing Levy imekataliwa. Kubalini yaishe ili tuweze kujenga Kenya kwa furaha na upendo bila ya kuwatoza wafanyikazi ushuru mwingi."
}