GET /api/v0.1/hansard/entries/1373802/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1373802,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373802/?format=api",
    "text_counter": 309,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": " Nitaongea. Hakuna shida. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie hili jambo. Kwanza, Katiba yetu imeruhusu kuwa na haki ya makao. Vilevile, sisi kama Chama cha Azimio, haki ya makao pia ilikuwa moja ya ajenda zetu. Kama vile Kiongozi wa Chama cha Walio Wachache, Mhe. Wandayi, alivyosema, haoni ni kwa nini pia mimi ninaunga mkono. Kwa nini ilikuwa tuende haraka kwenye jambo hili? Kwa shauri, jambo hili si kuwa ni mbaya. Lipo katika Katiba na pia katika ajenda yetu, na hivi sasa limeletwa. Ni sawa, lakini namna lilivyoletwa lazima liangaliwe. Kwa mfano, leo hii kwangu Mombasa pahali panaitwa Buxton, mpango huu ulifanywa na hata Rais akaja hapo. Nyumba zilivunjwa na kulikuwa na watu wanaoishi hapo. Vilevile, nyumba zilivunjwa Likoni kwa Mhe. Mishi. Juzi, kwa masikitiko makubwa ya mzee wetu, Mhe Omar Mwinyi, alifiliwa na bibi yake. Ndani ya wiki mbili akiwa anaomboleza, tingatinga zilivunja nyumba za watu wake wa Changamwe. Tulilaani kitendo kile sana. Mhe. Spika wa Muda, ndugu yangu, Mhe. Owen Baya, ambaye yupo hapa, anaijua Mombasa vizuri. Kama nilivyosema mwanzo, mpango huu haukuwa mbaya; lakini njia unavyofanywa ndio mbaya. Kwa nini nyumba zivunjwe Buxton, Likoni ama Changamwe? Pale Jomvu, kuna eneo kubwa la Serikali ambalo zamani lilikuwa likitumiwa kama holding The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}