GET /api/v0.1/hansard/entries/1373821/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1373821,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373821/?format=api",
"text_counter": 328,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": " Mtachukua muda wangu sana. Katika haya ninayosema, nilisikitika sana kwa sababu Jomvu na Changamwe ni kama mjomba na shangazi. Ni maeneo Bunge yaliyopakana. Katika mpango huu, Mhe. Omar Mwinyi, ambaye ni mjumbe wa hapo, leo akiwa katika maombolezi, watu wake wanavunjiwa nyumba. Jambo hilo halikuwa sawa. Lakini kama mjumbe wa Jomvu, kitendo kile tulikilaani kwa kuwa si cha ubinadamu, hata kama alikuwa anataka kufanya jambo lolote. Kwa hivyo leo, imani yangu inanituma. Wale wakaazi wa nyumba hizo, ilikuwa badala ya kuwa wapangaji, wakatiwe pesa pole pole ili wawe wamiliki baadaye, kuliko kuvunjia watu katika sehemu ambazo pia zina shauku. Leo nyumba zimevunjwa Buxton, na si ajabu kuwa pengine mwenye kufanya kazi alichukua hati miliki ya pale ambayo hakununua, akapeleka benki, akapata pesa kisha akajenga nyumba zile. Mahali kwingine pia ni vivyo hivyo. Leo ninauliza, 1.5 per cent ama moja nukta tano kwa 100 ambayo watu wanakatwa na waajiri… Hata wafanyi kazi wangu wanakatwa hiyo pesa. Mhe. Injendi amesema wakichelewa kidogo wameambiwa watakatwa 3 per cent . Hii levy ilipoanzishwa, ofisi yangu haikuwa na operating cash . Wafanyi kazi walikuja kwangu niwakopeshe pesa ya Housing Levy . Kama hali ni hiyo kwa wafanyakazi, je wale wengine ambao hawafanyi kazi, hali itakuwa gani? Lazima hali hii iangaliwe kwa sababu watu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}