GET /api/v0.1/hansard/entries/1373824/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1373824,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373824/?format=api",
    "text_counter": 331,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": "Kwa sababu inavyoendelea kuna uwezekano wa watu wengine kukatwa wakapata nyumba na wengine kukosa. Ikawa ni wengine kupanda kwa migongo ya wengine ili kufaidi na hali wengine wasifaidi. Sheria moja ni kuwa lazima uwe Mkenya. Dada yetu, Mhe. Irene Mayaka, aliuliza swali moja. Kama mtu anatoka mashambani na aende pale Pangani, Buxton ama pahali popote na kusema pia yeye ni Mkenya anataka nyumba, hiyo ni hali ya kuchanganyikiwa ya aina gani? Aliyeko pale aachwe na mwingine apewe. Hii inamaanisha hata yule aliyembali, kabla afikiwe atakuwa ashakufa, mwanawe na mjukuu wake pia akatwe ndio wafikiwe. Tuko na mzigo mkubwa na mwanzo lazima tuuangalie kabla ya kufanya haya. Tuko na deni la Standard Gauge Railway (SGR), Expressway, na madeni mengine kama Dongo Kundu. Mhe. Kimani Ichung’wah, Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni yuko hapa, na alikua Mwenyekiti wangu kwa Budget and Appropriations Committee. Leo mimi niko katika Kamati ya Kiidala ya Uchukuzi na Miundomisingi. Tunadaiwa Ksh1 bilioni na kampuni inaitwa Fujita Corporation ambayo imejenga Dongo Kundu. Kwa nini Ksh63 bilioni ambazo tumechukua kwa Housing Levy na hatujui itajenga nyumba gani isiende mwanzo kulipa madeni ndio kisha waangalie mambo mengine?"
}