GET /api/v0.1/hansard/entries/1373831/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1373831,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373831/?format=api",
    "text_counter": 338,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kikuyu, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Kimani Ichung’wah",
    "speaker": null,
    "content": " Asante Mhe. Spika wa Muda. Mhe. Bady Twalib amesema kuwa tuko na Ksh63 bilioni ambazo hazijulikani zitajenga manyumba wapi. Kwa hivyo, mbona tusitumie hizo fedha kulipa madeni ya pending bills ya wenye kandarasi wa Fujita Corporation, ambao wanajenga barabara huko Dongo Kundu katika eneo lake la Bunge. Lakini Mhe. Bady Twalib alipitisha sheria hapa na kusema hizi fedha za Housing Levy haziwezi kutumika kwa mahitaji mengine yoyote, hata kulipa madeni ila tu kazi ya ujenzi wa manyumba na mambo ambayo yanaambatana na huo ujenzi. Kwa hivyo, Mhe. Bady asiwafanye Wakenya waamini kuwa mimi ndiye nimekataza Fujita Corporation kulipwa. Sijui ako na nia gani na Fujita Corporation . Kufuatia Kanuni za Kudumu 90, atwambie anamjua aje huyu Fujita Corporation. Mbona anamtetea yeye tu alipwe?"
}