GET /api/v0.1/hansard/entries/1373836/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1373836,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373836/?format=api",
"text_counter": 343,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": " Sawa. Sina interest ama jambo lolote na Fujita Corporation. Nimetaja tu hali ilivyo. Nikiwa mwanakamati wa Kamati ya Kiidala ya Uchukuzi na Miundomisingi, ninajua ni wapi tunadaiwa, hatujamaliza kazi na hatuendelei mbele. Kununua nyumba hizi, inatakikana utoe asilimia kumi. Hii inamaanisha kama ni shilingi milioni tano uwe na Ksh500,000. Mama mboga na bodaboda watatoa Ksh500,000 wapi? Ninaona huu ni ufisadi unakuja. Kwa Mbunge Ksh5 milioni ni mswaki na kwa hivyo, Mbunge anaweza kuchukua pesa na kuweka arbuni ya nyumba kumi...."
}